Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

NFF yamuomba radhi rais wa Nigeria kwa kushindwa kufuzu Kombe la Dunia

NFF Pict

Muktasari:

  • Mechi ya tatu na wa mwisho hatua ya makundi itakuwa dhidi ya Uganda, Desemba 30, 2025. Mechi hizi zote zitafanyika kwenye Uwanja wa Complexe Sportif de Fès uliopo Mji wa Fès.

Shirikisho la Soka Nigeria (NFF), limeomba radhi Rais wa nchi hiyo, Bola Ahmed Tinubu na mashabiki wote wa soka nchini humo, kufuatia timu yao Super Eagles kushindwa kufikia lengo la kufuzu Kombe la Dunia 2026.

Matumaini ya Super Eagles kufuzu kwenye fainali hizo zitakazounguruma nchini Mexico, Marekani na Canada, yalivunjika ikipoteza mechi ya mchujo dhidi ya DR Congo iliyochomoza na ushindi wa penalti 4-3, baada ya sare ya bao 1-1 katika dakika 120.

Taarifa ya NFF imeanza kumuomba radhi Rais  Bola Ahmed Tinubu, kisha mashabiki wote wa soka ambao kwa muda wote walionyesha kuwa na timu yao, wakati wa msako wa tiketi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026.

Hata hivyo, NFF imeahidi kuandaa upya timu ya taifa, kwa lengo la kuwa na kikosi imara kwa ajili ya siku zijazo, ambapo wamedhamiria kuiona Super Eagles ikirejea kwa nguvu zaidi kwenye fainali za Kombe la Dunia.

NF 02

Aidha shirikisho hilo limebainisha kwamba, umakini wote kwa sasa unaelekezwa kwenye fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) zitakazofanyika nchini Morocco, Desemba, 2025.

Shirikisho limesema fainali hizo ni fursa ya kupoza machungu ya mashabiki wa Nigeria, pamoja na kuonyesha uthabiti ambao umekuwa ukitambulisha soka la nchi hiyo ya Afrika Magharibi.

Katika fainali za AFCON 2025, Nigeria imepangwa Kundi C na Tunisia, Uganda, na Tanzania. Hii inatoa changamoto muhimu kwa Nigeria kushindana ili kufuzu hatua ya 16 bora.

Kundi hili linaonekana kuwa na ushindani mkali, kwani timu zote zinajivunia wachezaji wenye uwezo na historia nzuri ya michuano ya AFCON, hivyo mashabiki wa Nigeria wanatarajia kuona mechi za kuvutia.

NF 01

Mechi ya kwanza ya Nigeria katika Kundi C itakuwa dhidi ya Tanzania, ambayo itafanyika Desemba 23, 2025.

Baada ya hapo itacheza dhidi ya Tunisia, Desemba 27, 2025. Hii itakuwa mechi muhimu kwani Tunisia ni mpinzani mwenye historia nzuri ya AFCON na ushindi au sare unaweza kuamua nafasi ya Nigeria katika msimamo wa kundi C.

Mechi ya tatu na wa mwisho hatua ya makundi itakuwa dhidi ya Uganda, Desemba 30, 2025. Mechi hizi zote zitafanyika kwenye Uwanja wa Complexe Sportif de Fès uliopo Mji wa Fès.