Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Newcastle: Mtupishe Isak, Bruno hawauzwi

Muktasari:

  • Hilo limegeuka ndani ya miezi 12, ambapo mwaka mmoja uliopita, Newcastle iliwaambia mashabiki wake isishangae ikiona moja ya mastaa wao wa maana wakiuzwa kwa sababu walikuwa wamekaliwa kooni na ishu ya usawa kwenye mapato ya matumizi.

NEWCASTLE, ENGLAND: MABOSI wa Newcastle United wamezipiga onyo kali klabu za Liverpool, Arsenal na Manchester City kuacha kuwasumbua kwa sababu mastaa wao Alexander Isak na Bruno Guimaraes hawauzwi.

Hilo limegeuka ndani ya miezi 12, ambapo mwaka mmoja uliopita, Newcastle iliwaambia mashabiki wake isishangae ikiona moja ya mastaa wao wa maana wakiuzwa kwa sababu walikuwa wamekaliwa kooni na ishu ya usawa kwenye mapato ya matumizi.

Lakini, sasa mkurugenzi mtendaji mkuu wa klabu hiyo, Darren Eales ameibuka na kudai kwamba hakuna mchezaji yeyote wa maana kwenye kikosi hicho cha Eddie Howe atapigwa bei kwenye dirisha lijalo la majira ya kiangazi.  Na sasa, wamiliki wa klabu hiyo, PIF ipo tayari kufungulia pochi mwisho wa msimu huu kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi ili kunasa huduma ya mastaa wapya.

Eales alifichua hesabu za kifedha za klabu hiyo kwa msimu uliopita kwamba imepata hasara ya Pauni 11.1 milioni - licha ya mapato yake kuongezeka kwa asilimia 28 kufikia Pauni 320.3 milioni - kiwango ambacho ni pungufu kwa Pauni 73.4 milioni ya mwaka uliopita.

Kwa hesabu hizo, Newcastle haipo kwenye hatari ya kukiuka kanuni za FFP za Ligi Kuu England, kwa maana hiyo kwamba timu hailazimiki tena kuuza wachezaji wake kupata pesa za kuweka sawa vitabu vyao.

Eales alisema: "Tuna dhamira na hitaji la kubakiza wachezaji wetu wote muhimu, wote wana mikataba mirefu. Kwa kusema hivyo, hiyo ina maana hatupo kwenye ulazima wa kufanya jambo lolote lile la kuuza. Tuna uongozi imara, unaotaka mambo mazuri ya klabu."