Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Neville awataja Arsenal, Man City mbio za ubingwa

NEVILLE
NEVILLE

Muktasari:

  • Kikosi cha Aston Villa kinachonolewa na Mhispaniola Unai Emery kipo nyuma kwa pointi tatu tu dhidi ya vinara Arsenal baada ya mechi 17, lakini nahodha wa zamani wa Manchester United, Neville hashawishiki na timu hiyo kama itaweza kushindana kwenye mbio za ubingwa hadi mwisho.

Neville awataja Arsenal, Man City mbio za ubingwa


LONDON, ENGLAND: GARY Neville anaamini mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England ni mbio za farasi wawili na hivyo kuwaweka kando Aston Villa kwenye mchakamchaka huo.

Kikosi cha Aston Villa kinachonolewa na Mhispaniola Unai Emery kipo nyuma kwa pointi tatu tu dhidi ya vinara Arsenal baada ya mechi 17, lakini nahodha wa zamani wa Manchester United, Neville hashawishiki na timu hiyo kama itaweza kushindana kwenye mbio za ubingwa hadi mwisho.

Aston Villa imeshinda mechi saba mfululizo kwenye Ligi Kuu England, ikiwamo dhidi ya Arsenal ya Mikel Arteta.

Lakini, Neville anaamini Arsenal inaweza kufanya jambo safari hii, ikiwa kileleni kwenye msimamo wa ligi wakati wa Krismasi.

Kocha huyo wa zamani wa Valencia amesema haishangazi kuona Man City ikiwa mshindani mkubwa wa Arsenal katika vita ya ubingwa. Kocha Guardiola na straika wake matata Erling Haaland ndiyo wanaonekana kuitisha Arsenal kwenye mbio hizo.

"Naweka mstari kwa timu mbili za juu," amesema Neville baada ya Aston Villa kuichapa Manchester United.

"Aston Villa ipo pale na wanastahili kupewa heshima, lakini hawawezi kushinda ubingwa. Nitashangaa sana kama hilo litatokea. Na hivyo bado mambo mengi yatakuwa yameenda kombo kwa Arsenal na Man City ili Aston Villa ibebe ubingwa.

"Ligi ina maajabu, nimesema inaweza zisiwe mbili za juu, bali ni zile za juu. Man City ni kawaida, wazuri sana kwenye hilo. Wanaye Erling Haaland na Pep Guardiola, watu spesho zaidi."