Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Napoli yakataliwa tena kwa Kobbie Mainoo

Muktasari:

  • Mainoo (20), ni zao la akademi ya United na amekuwa sehemu muhimu ya mipango ya muda mrefu ya klabu hiyo lakini tangu kuwasili kwa Amorim msimu uliopita hali inaonekana tofauti kwake.

KIUNGO wa Manchester United, Kobbie Mainoo hataruhusiwa kuondoka Old Trafford dirisha la usajili la Januari baada ya Kocha Ruben Amorim kuweka msimamo mkali wa kumbakisha, licha ya kuwepo kwa ofa kutoka Napoli ya Italia.

Mainoo (20), ni zao la akademi ya United na amekuwa sehemu muhimu ya mipango ya muda mrefu ya klabu hiyo lakini tangu kuwasili kwa Amorim msimu uliopita hali inaonekana tofauti kwake.

Kocha amekuwa akidai Mainoo hafanyi baadhi ya mambo ambayo anamwambia, ndiyo maana amekuwa akimweka benchi mara kwa mara lakini mara kadhaa ambazo zimekuja ofa kutoka timu zinazomhitaji tangu dirisha lililopita, amekuwa akizuia asiuzwe.

Mbali na Napoli, Chelsea na Bayern Munich zinaonekana pia kuhitaji huduma ya staa huyu anayetamani sana kuondoka ili kupata timu itakayompa nafasi ya kucheza jambo litakalosaidia pengine kuitwa timu ya taifa ya England kuelekea michuano ya Kombe la Dunia mwakani.

Mkataba wa Mainoo unatarajiwa kumalizika mwaka 2027, na msimu huu amecheza mechi 11 za michuano yote.


Jan Paul van Hecke

TOTTENHAM Hotspur ipo tayari kusubiri hadi dirisha lijalo la majira ya kiangazi ili kumsajili beki wa Brighton & Hove Albion, Jan Paul van Hecke, raia wa Uholanzi mwenye umri wa miaka 25. Van Hecke ameonyesha kiwango cha juu katika safu ya beki ya Brighton, tangu msimu uliopita hali iliyozivutia timu nyingi. Spurs inaamini ikisubiri hadi dirisha la majira ya kiangazi itakuwa na nafasi nzuri ya kumpata beki huyo kwa gharama nafuu zaidi, kwa sababu mkataba wake utakuwa umebakisha mwaka mmoja.


Brennan Johnson

WINGA wa Tottenham Hotspur, Brennan Johnson yupo kwenye orodha ya wachezaji wanaowindwa na Crystal Palace inayotaka kuimarisha safu yao ya ushambuliaji dirisha la usajili la Januari. Johnson, 24, alijiunga na Spurs akitokea Nottingham Forest mwaka 2023, lakini amekuwa hana nafasi ya kudumu kikosi cha kwanza, jambo linalofanya klabu hiyo kufikiria kumwachia ikiwa itapata ofa itakayoridhisha. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2028. Msimu huu amecheza mechi 20 za michuano yote lakini nyingi amekuwa akiingia akitokea benchi.


Dusan Vlahovic

BARCELONA inatajwa kujiondoa tararibu katika mchakato wa kumwania mshambuliaji wa Juventus na timu ya taifa ya Serbia, Dusan Vlahovic, 25. Staa huyu sasa anatajwa kuwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kujiunga na AC Milan ambayo bado inapambana kutaka kumsajili.

Vlahovic amekuwa akihusishwa kwa muda mrefu na Barca, lakini changamoto za kifedha za klabu hiyo pamoja na vipaumbele vingine vya usajili zimeifanya iachane na mpango wa kutaka kumsajili. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwakani.


Dayot Upamecano

REAL Madrid na Paris Saint-Germain zinaonyesha nia ya kumsajili beki wa Bayern Munich na timu ya taifa ya Ufaransa, Dayot Upamecano, mwenye umri wa miaka 27. Hata hivyo, Bayern Munich hawako tayari kumuacha kwa urahisi na badala yake inapanga kuanza mazungumzo ya mkataba mpya ili kumbakisha Allianz Arena ikiwa atakubali kufanya hivyo. Upamecano ni miongoni mwa mabeki tegemeo wa Bayern na mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwakani.


Igor Thiago

TOTTENHAM Hotspur, Aston Villa na West Ham United zimeingia kwenye vita kali ya kuiwania saini ya mshambuliaji wa Brentford, Igor Thiago, raia wa Brazil mwenye umri wa miaka 24. Brentford haina mpango wa kumwachia fundi huyu kwani bado ni sehemu ya mipango yao ya muda mrefu lakini inaweza kufikiria kufanya hivyo ikiwa itapokea ofa nono. Tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 17 za michuano yote na kufunga mabao 12. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2029.


Manuel Ugarte

MANCHESTER United inapanga kusikiliza ofa zitakazowasilishwa kwa ajili ya kiungo wao wa kimataifa wa  Uruguay, Manuel Ugarte, 24,  dirisha la usajili la Januari. Ugarte alijiunga na Man United huku mashabiki wa timu hiyo wakiwa na matarajio makubwa juu yake, lakini bado hajajijengea nafasi ya kudumu kikosi cha kwanza kutokana na ushindani mkubwa wa namba wa eneo la kiungo. Mkataba wake na United unatarajiwa kumalizika mwaka 2029.


Niclas Fullkrug

AC Milan ipo tayari kuharakisha mchakato wa kumsajili mshambuliaji wa West Ham United, Niclas Fullkrug, 32, ili kumpata dirisha lijalo la majira ya baridi. Milan imepata matumaini makubwa ya kufanikisha usajili huo baada ya mshambuliaji huyo Mjerumani kuonyesha wazi nia ya kuondoka West Ham, akitafuta changamoto mpya pamoja na nafasi zaidi ya kucheza. Fullkrug ni miongoni mwa mastaa wenye uzoefu mkubwa  Ulaya, jambo linalomfanya kuwa chaguo la muda mfupi kwa Milan inayotaka kumpata hata kwa mkopo wa nusu msimu.