Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nani Arsenal? Kiboko mipira iliyokufa ni hawa

BACK Pict

Muktasari:

  • Kocha Mikel Arteta na benchi lake la ufundi, hasa kocha wa mipira ya adhabu, Nicolas Jover, wameifanya mipira hiyo kusimama kuwa moja ya silaha hatari zaidi za kufunga mabao kwa vigogo hao wa Emirates.

LONDON, ENGLAND: ARSENAL imekuwa ikisifiwa sana kwa ufanisi wao mkubwa katika mipira ya adhabu.

Kocha Mikel Arteta na benchi lake la ufundi, hasa kocha wa mipira ya adhabu, Nicolas Jover, wameifanya mipira hiyo kusimama kuwa moja ya silaha hatari zaidi za kufunga mabao kwa vigogo hao wa Emirates.

Kwa kweli, hakuna timu yoyote ya Ligi Kuu England iliyofunga mabao mengi zaidi kupitia mipira ya adhabu msimu huu kuliko Arsenal, ikiwa na mabao 17, zaidi ya wapinzani wao wa karibu Manchester United ambao wamefunga mara 14 kwa staili hiyo ya mipira ya adhabu.

BAC 01

Arsenal pia ni mahiri katika kujilinda dhidi ya mipira ya adhabu, ikiruhusu mabao matano pekee msimu huu hadi sasa, sawa na Everton na Tottenham Hotspur, na wakizidiwa tu na Brentford iliyoruhusu mabao manne pekee.

Hata hivyo, inageuka kuwa Arsenal inaoongoza msimamo wa ligi siyo timu bora zaidi katika kufunga mabao kutokana na mipira ya adhabu kwa ufanisi.

BAC 04

Rekodi hiyo inashikiliwa na Man United. Licha ya mapungufu mengi ambayo Mashetani Wekundu walikuwa nayo chini ya kocha wa zamani Ruben Amorim, jambo moja lililoboreshwa kwa kiasi kikubwa ni uwezo wao wa kuwa tishio kupitia mipira ya adhabu.

Man United imebadilika kutoka kuwa dhaifu sana katika kona na mipira ya adhabu hadi kuwa miongoni mwa timu bora zaidi Ligi Kuu England msimu huu, mwenendo ambao umeendelea chini ya kocha wa muda, Michael Carrick, hasa baada ya bao la kwanza la Casemiro dhidi ya Fulham, Jumapili iliyopita.

BAC 02

Kama ilivyotajwa, Man United iko nafasi ya pili nyuma ya Arsenal kwa idadi ya jumla ya mabao ya mipira ya adhabu, huku mabao 10 waliyofungwa yakiwa yanawaweka nafasi ya nane kwa wastani katika kujilinda dhidi ya mipira hiyo.

Lakini, linapokuja suala la ufanisi wa kutumia mipira iliyokufa, hakuna timu inayowazidi Man United katika ligi. Takwimu kutoka The Athletic zinaonyesha kuwa Man United hufunga mabao manane kwa kila mipira 100 ya adhabu iliyopata msimu huu.

BAC 03

Licha ya Arsenal kuitwa mara kwa mara “Set Pieces FC”, wao wanashika nafasi ya pili kwa kipimo hiki kwa kufunga mabao 7.3 kwa kila mipira 100 ya adhabu.

Wapinzani watatu wa London, Chelsea, Tottenham na Fulham wanakamilisha tano bora, wakifunga kwa wastani wa mabao 6.7, 5.7 na 5.5 kwa kila mipira 100 ya adhabu mtawalia. Newcastle, Leeds na Aston Villa ndizo timu nyingine pekee zinazofunga zaidi ya bao moja kwa kila mipira 20 ya adhabu, zikiwa na wastani wa mabao 5.1 kwa kila mipira 100.

Upande wa pili wa jedwali, Brentford ndiyo timu dhaifu zaidi katika ufanisi wa kufunga kupitia mipira ya adhabu. Kocha wa Brentford, Keith Andrews, aliteuliwa majira ya joto baada ya kuondoka kwa Thomas Frank, akiwa hapo awali kocha wa mipira ya adhabu wa klabu hiyo.

BAC 05

Hata hivyo, utaalamu huo haujaonekana kuleta matunda kwani Brentford hufunga mabao 1.9 pekee kwa kila mipira 100 ya adhabu wanayopata.

Wolves, iliyopo mkiani mwa msimamo wa Ligi Kuu England, pia iko karibu na mwisho wa jedwali kwa ufanisi wa mipira ya adhabu, ikifunga mabao 2.5 kwa kila mipira 100.

Kama kungekuwa na kushuka daraja kwa kipimo hiki, basi Nottingham Forest ndiyo timu ambayo ingeshuka daraja kwa mabao 3.3 kwa kila mipira 100 ya adhabu.

Na cka kushangaza, Liverpool iko juu kidogo tu kwa mabao 3.4, na pia wanazidiwa na wapinzani wao wa mtaa, Everton wenye mabao 3.5.

Manchester City nayo ipo katika nusu ya chini ya jedwali hili, ikifunga mabao 3.8 kwa kila mipira 100 ya adhabu, ikiwa kati ya Burnley (3.6) na Sunderland (4.0).