Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Droo ya UEFA eti mpango umepangwa!

Muktasari:

  • Timu 16 zilizofuzu hatua ya mchujo sasa zimefahamu hatima yao baada ya kila moja kutambua itamenyana na nani katika mchujo huo.

ZURICH, USWISI: MASHABIKI wa soka wameibuka na kudai kuwa droo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya imepangiliwa kimpango mpango baada ya Real Madrid kuchaguliwa kucheza dhidi ya Benfica katika mechi ya mchujo wa kuwania kuingia kwenye hatua ya 16 bora.

Timu 16 zilizofuzu hatua ya mchujo sasa zimefahamu hatima yao baada ya kila moja kutambua itamenyana na nani katika mchujo huo.

Pia zinajua upande gani wa droo itakazokuwa, lakini baadhi ya mashabiki wanaamini mchakato mzima ulikuwa umeandaliwa mapema.

Hii ni kwa sababu Real Madrid kupangwa kukutana na Benfica ya Jose Mourinho.

Benfica iliifunga Real Madrid kwa mazingira ya kusisimua Jumanne iliyopita katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi iliyochezwa kwa mtindo wa ligi, ambapo kipa Anatoliy Trubin alifunga bao katika dakika za majeruhi kuisaidia timu yake kufuzu hatua ya mchujo kwa tofauti ya mabao.

Baadhi ya mashabiki wanaamini ni bahati mbaya isiyo ya kawaida kwa timu hizo mbili ambazo kila moja ilikuwa na nafasi ya asilimia 50 kukutana, kupangwa tena dhidi ya nyingine katika raundi iliyofuatia, muda mfupi baada ya kumenyana.

Timu itakayofuzu kutoka katika mchuano huo itakutana na ama Sporting CP au Manchester City katika hatua ya 16 bora. Mabingwa watetezi Paris Saint-Germain, kwa upande wao, watakutana na wapinzani wao wa Ligue 1, AS Monaco.

PSG inaweza kisha kukutana na aidha Barcelona au Chelsea, ambao hawatapangwa dhidi ya Newcastle au Qarabag. Kikosi cha kocha Diego Simeone, Atletico Madrid, kimepangwa kukutana na Club Brugge ya Ubelgiji, huku Mabingwa wa Ugiriki, Olympiacos, watavaana na Bayer Leverkusen.

Borussia Dortmund wamepangwa kucheza dhidi ya Atalanta, huku wapendwa wa Norway, Bodoe/Glimt, wakipata pambano kali dhidi ya Inter Milan.

Shabiki mmoja aliandika: “Droo ya Benfica dhidi ya Real Madrid ilikuwa imepangiliwa sana, lakini niko tayari kuifurahia.”

Mwingine aliongeza: “Hii ni droo iliyopangwa. Hakuna mjadala.”

Shabiki wa tatu aliaandika: “Sijawahi kuona droo iliyopangwa waziwazi kama hii.”

Na mwingine alikomenti: “HII LAZIMA iwe imepangiliwa.”

Ratiba hii si tu marudio ya mechi ya kusisimua ya wiki hii, bali pia inamkutanisha Mourinho na klabu kubwa aliyowahi kuinoa.

Mreno huyo maarufukama The Special One, aliinoa Real Madrid kuanzia 2010 hadi 2013, kipindi ambacho alishinda LaLiga na Kombe la Copa del Rey.

Hata hivyo, hakuna ushahidi wala dalili zozote kwamba droo hiyo ilipangwa kwa namna yoyote ile.

Mechi za mchujo zitachezwa Februari 17 na 18, huku michezo ya marudiano ikichezwa wiki moja baadaye Februari 24 na 25.