Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kompyuta inasema... We nani ubishe, Arsenal bingwa EPL

Muktasari:

  • The Gunners ilipata pigo katika mbio za ubingwa baada ya kupoteza kwa kishindo cha 3-2 dhidi ya Man United kwenye Uwanja wa Emirates.

LONDON, ENGLAND: ARSENAL itatwaa ubingwa wa Ligi Kuu England licha ya kupoteza dhidi ya Manchester United Jumapili, kwa mujibu wa utabiri wa kompyuta maalumu.

The Gunners ilipata pigo katika mbio za ubingwa baada ya kupoteza kwa kishindo cha 3-2 dhidi ya Man United kwenye Uwanja wa Emirates.

Jurrien Timber alimbabatiza beki Lisandro Martinez na kujifunga kuipatia Arsenal bao la kuongoza dakika ya 30 kabla ya Bryan Mbeumo kusawazisha baada ya kosa la Martin Zubimendi, aliyejaribu kupiga pasi ya nyuma kwa kipa David Raya na hivyo mpira huo kuwahiwa na Mcamerooni, Mbeumo.

Patrick Dorgu kisha aliiongoza Manchester United mbele kwa bao la kuvutia muda mfupi baada ya kipindi cha pili kuanza, wakati alipogongeana pasi moja moja na Bruno Fernandes na kufumua shuti la guu la kushoto lililomshinda kipa, Raya.

Mtokea benchini Mikel Merino alidhani ameokoa pointi moja kwa Arsenal dakika ya 84, wakati alipofunga baada ya kutokea purukushani kwenye goli la Man United kufuatia mpira wa kona, lakini Matheus Cunha alifunga bao la ushindi la dakika za mwisho na kuwaumiza wapambanaji wa ubingwa.

Licha ya kichapo hicho, supercomputer kutoka Aceodds bado inatabiri kuwa Arsenal itatwaa taji la Ligi Kuu England msimu huu, ambapo mara ya mwisho ilinyakua taji hilo msimu wa 2003/04 ilipocheza bila ya kupoteza mchezo wowote kwenye ligi.

Supercomputer hiyo, iitwayo BETSiE, imetabiri Arsenal itamaliza msimu ikiwa na jumla ya pointi 83, saba zaidi ya Manchester City watakaomaliza nafasi ya pili katika msimamo wa mwisho wa msimu. Hilo linaaminisha msimu utamalizika kwa utulivu mkubwa kwa kocha Mikel Arteta na kikosi chake.

Kwa Arsenal na Man City kuchukua nafasi mbili za juu, Aston Villa imetabiriwa itamaliza nafasi ya tatu ikiwa na pointi 68.

Nao Manchester United wanatarajiwa kumaliza nafasi ya nne, licha ya mwanzo dhaifu wa msimu chini ya Ruben Amorim, ambaye alifukuzwa kazi mapema mwezi huu. Kwa mujibu wa supercomputer hiyo, Chelsea itamaliza nafasi ya tano huku Liverpool ikiwa kwenye namba sita.

Newcastle United, Brentford, Fulham na Brighton wanatarajiwa kufuata, na hivyo kukamilisha nusu ya juu ya msimamo wa ligi hiyo.

Tottenham Hotspur imetabiriwa kupitia tena mwisho mbaya wa msimu, kwamba itamaliza kwenye nafasi ya 15.

Kwa upande mwingine, timu zilizopanda daraja Sunderland na Leeds United zinatarajiwa kubaki Ligi Kuu England, zikimaliza nafasi ya 14 na 16 mtawalia.

Supercomputer pia imetabiri kuwa Wolves, Burnley na West Ham United zitashuka daraja na kwenda kwenye Championship mwishoni mwa msimu.

Nottingham Forest itaepuka kushuka daraja kwa kumaliza na pointi 44, tisa zaidi ya West Ham United watakaomaliza kwenye nafasi ya 18.

West Ham imepewa asilimia 83.8 ya kushuka daraja, huku Burnley ikipewa nafasi ya asilimia 99, na Wolves karibu hakika kushuka kwa asilimia 99.6, kwa mujibu wa supercomputer hiyo.