Nani abaki, aondoke Arsenal

Muktasari:
- Kwenye dirisha la mwisho la majira ya kiangazi katika zama za Edu, Arsenal ilifanya usajili wa mastaa watatu tu - ikiwamo uhamisho wa jumla wa kipa David Raya, ambaye mwanzoni alikuwa kwenye kikosi chao kwa mkopo, huku usajili mwingine wa wachezaji wawili waliofanya katika dirisha hilo la mwaka jana, iliwanasa kwa mkopo.
LONDON, ENGLAND: BAADA ya kushuhudia majeruhi wakitibua mbio za ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu, Arsenal inaweza kuchukua uamuzi wa kupangua kikosi kwa kuondoa baadhi ya mastaa na kuleta wengine wapya kwenye dirisha lijalo la majira ya kiangazi.
Kwenye dirisha la mwisho la majira ya kiangazi katika zama za Edu, Arsenal ilifanya usajili wa mastaa watatu tu - ikiwamo uhamisho wa jumla wa kipa David Raya, ambaye mwanzoni alikuwa kwenye kikosi chao kwa mkopo, huku usajili mwingine wa wachezaji wawili waliofanya katika dirisha hilo la mwaka jana, iliwanasa kwa mkopo.
Lakini, iliingiza zaidi ya Pauni 70 milioni pamoja na nyongeza nyingine za bonasi kwa kuwauza mastaa wake iliyowatoa kwenye akademia ambao ni Eddie Nketiah na Emile Smith Rowe, ikiwa ni miongoni mwa iliyowauza.
Sasa mrithi wa Edu, atakuwa na kibarua kizito cha kufanya usajili dirisha lijalo la majira ya kiangazi na kwa sasa inaelezwa, Andrea Berta ndiye anayepewa nafasi kubwa ya kwenda kuongoza idara hiyo ya kuuza na kununua mastaa Emirates.
Kama atateuliwa mwezi huu, basi atakuwa na muda mchache wa kujiandaa kuanza kufikiria ni mchezaji gani wa kuja kuongeza nguvu kwenye kikosi ili kiwe cha kiushindani msimu ujao.
Kutokana na mtangulizi wake, Edu kupata sifa kubwa kwa aina ya wachezaji aliowasajili na wale aliowaondoa kuifanya timu hiyo kuwa na nguvu na kushindania mataji, mrithi huyo atakuwa na kazi kubwa ya kuamua nani atoke na nani abaki kabla ya kuingia sokoni kusajili mchezaji mpya. Kuna wachezaji kibao wanahusishwa na Arsenal, wakiwamo mastraika, ambao wamekuwa wakitajwa mara kwa mara kama vile Benjamin Sesko na Alexander Isak.
Lakini, kwa sasa kitu kinachotazamwa ni wachezaji waliopo wanaounda kikosi cha Arsenal, je ni nani anapaswa kubaki na yupi wa kufunguliwa mlango wa kutokea kwenye dirisha lijalo la usajili? Kocha Arteta anataka kuwa na timu itakayokuwa na uwezo wa kushinda ubingwa wa Ligi Kuu England msimu ujao endapo kama itashindikana msimu huu.
David Raya - ABAKI
Neto - AONDOKE
Karl Hein - AONDOKE
William Saliba - ABAKI
Ben White - ABAKI
Gabriel - ABAKI
Jurrien Timber - ABAKI
Jakub Kiwior - ONDOKE
Oleksandr Zinchenko - AONDOKE
Takehiro Tomiyasu - ABAKI
Riccardo Calafiori - ABAKI
Myles Lewis-Skelly - ABAKI
Nuno Tavares - AONDOKE
Thomas Partey - AONDOKE
Martin Odegaard - ABAKI
Jorginho - AONDOKE
Mikel Merino - ABAKI
Declan Rice - ABAKI
Albert Sambi Lokonga - AONDOKE
Fabio Vieira - AONDOKE
Ethan Nwaneri - ABAKI
Reiss Nelson - AONDOKE
Marquinhos - AONDOKE
Kai Havertz - ABAKI
Bukayo Saka - ABAKI
Gabriel Jesus - ABAKI
Gabriel Martinelli - ABAKI
Leandro Trossard - ABAKI
Raheem Sterling - AONDOKE