Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nani aanika matatizo Man United, asema kuna kitu msimu huu

NANI Pict
NANI Pict

Muktasari:

  • Man United inapitia wakati mgumu chini ya kocha Ruben Amorin baada ya kumaliza nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligi ya EPL msimu uliopita, huku msimu huu ikianza vibaya kwa kushinda mechi mbili, kufungwa tatu na sare moja.

Winga wa zamani wa Manchester United, Luís Carlos Almeida da Cunha ‘Nani’ ameonyesha kuwa na matumaini na klabu hiyo tofauti na matarajio ya magwiji wengine waliowahi kutoa maoni yao, kuhusu mustakabali wa Mashetani Wekundu msimu huu 2025-2026.

Man United inapitia wakati mgumu chini ya kocha Ruben Amorin baada ya kumaliza nafasi ya 15 kwenye msimamo wa Ligi ya EPL msimu uliopita, huku msimu huu ikianza vibaya kwa kushinda mechi mbili, kufungwa tatu na sare moja.

Nani, ambaye aliwahi kuitumikia timu ya taifa ya Ureno, amesema kinachoendelea Man united kwa sasa anaamini ni hali ya mpito, lakini mambo yatakaa sawa na huenda msimu huu kukawa na mabadiliko, tofauti na msimu uliopita.

Katika mahojiano wakati wa Mkutano wa Soka wa Ureno 2025, Nani amesema kuwa mabadiliko ya mara kwa mara ya wachezaji yameiathiri kwa kiasi kikubwa timu hiyo ambayo iliwahi kutamba katika soka la ndani nan je ya England.

NAN 01

Ameeleza kuwa, kikosi cha sasa hakifahamu vizuri falsafa na utamaduni wa klabu hiyo.

“Ndiyo, nadhani kilichobadilika ni idadi ya wachezaji wasiozoea kucheza katika klabu hiyo. Zamani, ukibadilisha mchezaji mmoja au wawili, walijiunga na wachezaji waliopo na walijifunza haraka. 

“Sasa unabadilisha karibu kikosi chote na hawajui falsafa za klabu. Inachukua muda kuelewa nini kinachotakiwa, jinsi klabu inavyofanya kazi na jinsi mashabiki wanavyofikiri. Sijui kama wataelewa jinsi ya kuichezea klabu hiyo. Nadhani hiyo ndiyo sababu ya ukosefu wa mafanikio.” amesema.

Nani ameongeza kuwa licha ya hali hiyo, anaamini Manchester United inaelekea kwenye kizazi kipya chenye mazingira mapya na muda si mrefu hali hiyo itaanza kuonekana.

“Ninaamini kuna kitu kinatengenezwa, klabu inaunda kizazi kipya, inaunda mazingira mapya. Ninaamini kupitia haya mabadiliko mapya, Man United itafanikiwa.”

Licha ya kutoa tathmini ya ukosoaji kuhusu hali ya sasa ya Manchester United, Nani ameelezea matumaini kwamba timu hiyo inaweza kubadilika na kufanya vizuri msimu huu.

“Kwa kweli, nilikuwa na hisia nzuri kwa msimu huu, matarajio mazuri kwa sababu tulijua tunahitaji kusajili wachezaji wapya na tumefanya hivyo. Tunajaribu kujenga timu imara,” amesema.

“Ligi Kuu ya England si rahisi. Ili kupata matokeo bora na kushinda mechi nyingi mfululizo, inahitaji muda. Lakini naamini katika mchakato huu. Timu ina vipaji vizuri, wachezaji na wazuri. Ni suala la muda.

NAN 02

“Kwa bahati mbaya, kila timu ni kali kwa sasa. Si kama zamani. Sasa unaona hata timu ndogo zinashindana vikali. Wachezaji wana nguvu, kasi, na ujuzi,” amesema.

Manchester United ilishinda mechi yao ya mwisho kwa mabao 2-0 dhidi ya Sunderland, na inatarajiwa kucheza dhidi ya Liverpool mara baada ya mapumziko ya mechi za kimataifa.

Nani aliichezea Manchester United kuanzia 2007 hadi 2015, na katika kipindi hicho alishinda mataji ya Ligi Kuu ya England (Premier League) na UEFA Champions League.