Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nagelsmann kocha mpya Ujerumani

BERLIN, UJERUMANI. JULIAN Nagelsmann ameteuliwa kuwa kocha mpya wa Ujerumani baada ya Hansi Flick kutimuliwa mapema mwezi huu baada ya kufungwa mabao 4-1 na Japan kwenye mchezo wa kirafiki.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 36 aliacha kazi Bayern Munich mapema mwaka huu, huku Thomas Tuchel akichukua nafasi yake Allianz Arena.

Nagelsmann alikuwa bado yupo chini ya mkataba na mabingwa hao wa Bundesliga hadi 2026, lakini Bavarians na Shirikisho la Soka la Ujerumani wamefikia makubaliano kwamba kocha huyo atainoa Ujerumani kuelekea michuano ya Euro 2024.

Flick alishinda mechi 12 kati ya 25 akiwa na Ujerumani ambayo alitua kuchukua mikoba ya Joachim Low mwaka 2021, ambaye aliwahi kufanya naye kazi kuanzia mwaka 2006 hadi 2014.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 58 aliiongoza Ujerumani kushinda mechi nane mfululizo alipoteuliwa, lakini Ujerumani ilifanya vibaya kwenye fainali za Kombe la Dunia 2022  yaliyofanyika Qatar.

Ujerumani ilikomea hatua ya makundi katika fainali hizo za Qatar baada ya kuwachapa Costa Rica kabla ya kutoka sare na Hispania na kuchapwa na Japan.