Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nabi aichapa Orlando 2-1, aipeleka Kaizer Chiefs kimataifa

Muktasari:

  • Kaizer Chiefs inayofundishwa na Kocha Nasreddine Nabi akiwa na wasaidizi wake, Khalil Ben Youssef na Cedric Kaze ambao wote walikuwa Yanga SC, imetwaa ubingwa huo kwa mara ya kwanza tangu ilipofanya hivyo msimu wa 2012-13 ikiwa ni takribani miaka 10 imepita huku ikiwa ni mara ya 14 katika historia yao.

USHINDI wa mabao 2-1 ilioupata Kaizer Chiefs maarufu AmaKhosi na kunyakua Kombe la Nedbank, umeifanya timu hiyo kufuzu michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika msimu ujao.

Kaizer Chiefs inayofundishwa na Kocha Nasreddine Nabi akiwa na wasaidizi wake, Khalil Ben Youssef na Cedric Kaze ambao wote walikuwa Yanga SC, imetwaa ubingwa huo kwa mara ya kwanza tangu ilipofanya hivyo msimu wa 2012-13 ikiwa ni takribani miaka 10 imepita huku ikiwa ni mara ya 14 katika historia yao.

Katika mchezo huo wa fainali uliochezwa leo Jumamosi Mei 10, 2025 kwenye Uwanja wa Moses Mabhida jijini Durban, Kaizer Chiefs ilionyesha kiwango cha juu na kuwachapa wapinzani wao wakubwa, Orlando Pirates.

Nahodha wa AmaKhosi, Yusuf Maart, alifunga bao la ushindi dakika ya 80 kwa shuti kali baada ya kupokea krosi kutoka kwa Ashley Du Preez.

Katika mchezo huo wa kusisimua wa Soweto Derby, Kaizer Chiefs ilionekana kuwa hatari zaidi kipindi cha pili kutokana na kushambulia kwa kasi.

Licha ya kuwa katikati ya msimamo wa Ligi Kuu ya Afrika Kusini ikishika nafasi ya tisa na pointi 30 baada ya kucheza mechi 26 huku ikishindwa kupata ushindi mechi zao saba za mwisho za ligi, Kaizer Chiefs ilionesha sura tofauti katika mchezo huu wa fainali.

AmaKhosi ilipata bao la kuongoza dakika ya 10 kupitia penalti iliyofungwa na Gaston Sirino, kufuatia beki wa Orlando Pirates, Deano van Rooyen, kuonekana kumfanyia faulo mchezaji wa Kaizer Chiefs, Pule Mmodi, ndani ya eneo la hatari.

Ingawa faulo hiyo ilionekana kuwa nyepesi, lakini Sirino hakufanya makosa, alimtesa kipa Sipho Chaine wa Orlando Pirates na kuuweka mpira nyavuni.

Orlando Pirates ilijibu mapigo dakika kumi baadaye kupitia bao la kichwa lililofungwa na Evidence Makgopa baada ya kupokea mpira uliopigwa kwa ustadi na Deon Hotto.

Hata hivyo, kipindi cha pili Orlando Pirates ilishindwa kutengeneza nafasi nyingi huku Kaizer Chiefs ikionekana kuwa hatari zaidi kupitia mashambulizi ya kushtukiza. Shinikizo lilizidi kwa Orlando Pirates na hatimaye safu yao ya ulinzi iliruhusu bao dakika ya 80 wakati Kaizer Chiefs ilipoanzisha shambulizi la haraka la 3v3.

Ilikuwa inaonekana kama nafasi hiyo imepotea lakini Du Preez alitoa krosi safi iliyomkuta Maart aliyekuwa akikimbia kutoka nyuma, shuti lake kali kwa mguu wa kushoto alilopiga ndani ya boksi mpira ukatikisa nyavu na kuwapa AmaKhosi kombe.

Baada ya mchezo huo wa fainali, Orlando Pirates ambayo iko nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi, haina muda wa kupumzika kwani inarejea uwanjani Jumanne ijayo kucheza dhidi ya Golden Arrows. Kaizer Chiefs itasubiri hadi Jumamosi ijayo kukabiliana na Sekhukhune United kwenye mchezo wa ligi