Mziki wa Man United unavyosukwa pale kati
Muktasari:
- Kocha huyo Mreno anaamini kwenye dirisha lijalo la Januari anaweza kunasa huduma ya kiungo mmoja kabla ya kuleta mastaa wengine matata kwenye eneo hilo la katikati ya uwanja litakapofikia dirisha kubwa la usajili, mwisho wa msimu.
MANCHESTER, ENGLAND: RUBEN Amorim anapambana kufumua safu ya kiungo ya kikosi cha Manchester United kuhakikisha kinakuwa bora kwa ajili ya kushindana na wababe wengine kwenye mchakamchaka wa mataji mbalimbali ikiwamo Ligi Kuu England.
Kocha huyo Mreno anaamini kwenye dirisha lijalo la Januari anaweza kunasa huduma ya kiungo mmoja kabla ya kuleta mastaa wengine matata kwenye eneo hilo la katikati ya uwanja litakapofikia dirisha kubwa la usajili, mwisho wa msimu.
Bruno Fernandes ataendelea kuwa sehemu muhimu ya kiungo ya Man United, wakati veterani Mbrazili Casemiro naye amekuwa msaada mkubwa kwa siku za hivi karibuni licha ya umri wake kuelekea miaka 34. Na Mason Mount amekuwa akiongeza kitu kwenye eneo hilo la kiungo tangu aliponaswa kwa Pauni 60 milioni akitokea Chelsea.
Lakini, Amorim anafahamu wazi eneo hilo bado lina shida kwenye kikosi chake. Manuel Ugarte na Diogo Dalot bado hawapo kwenye viwango vinavyotosha, huku Kobbie Mainoo kiwango chake kimeshuka kwa kasi kwa siku za hivi karibuni.
Kabla ya kukubali kibarua cha kuinoa Man United, Amorim alisema alikuwa akiifuatilia timu hiyo tangu alipokuwa kijana mdogo. Hivyo, anajua wazi mafanikio makubwa ya timu ya Man United yalianzia kwenye uimara wa safu ya kiungo.
Kama katika kipindi cha kocha Sir Alex Ferguson, safu yake ya kiungo ilikuwa na watu kama Roy Keane, Nicky Butt, Paul Scholes na David Beckham. Na wanne hao walikuwa wakipata msaada kutoka kwa Ryan Giggs. Safu hiyo ndiyo iliyobeba Mataji Matatu mwaka 1999 na mataji mengine kibao. Kocha Fergie pia aliwahi kuwa na watu kama Bryan Robson na Paul Ince waliokuwa mabosi kwenye eneo hilo la kiungo. Amorim naye anataka kuwa na watu kama Robson na Keane kwenye kiungo.
Kutokana na hilo, Amorim atahitaji pesa za kutosha za kusajili kuanzia kwenye dirisha lijalo na la majira ya kiangazi.
Mabosi wa Man United alitumia pesa nyingi kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi kuboresha safu ya ushambuliaji. Na katika kuelekea dirisha lijalo la usajili, mkurugenzi wa soka wa klabu hiyo, Jason Wilcox anafanya kazi kwa ukaribu na kocha Amorim katika kutimiza malengo ya kunasa viungo wa shoka kwenye kikosi hicho cha Old Trafford.
Viungo waliopo kwenye rada za Man United ni Carlos Baleba wa Brighton, Adam Wharton wa Nottingham Forest, Joao Gomes wa Wolves na staa wa VFB Stuttgart, Angelo Stiller. Kocha Amorim, anahitaji viungo vijana, wenye nguvu na viwango bora. Hata hivyo, hakuna wa bei ndogo, mfano Baleba anathaminishwa kwa Pauni 115 milioni.
Mmiliki mwenza wa Man United, bilionea Sir Jim Ratcliffe alisema anaamini kocha Amorim ataiweka sawa timu hiyo ndani ya miaka mitatu na ndio maana uwekezaji unaendelea kufanyika kwenye