Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtoto wa Buffon kuchezea Jamhuri ya Czech

BUFFON Pict

Muktasari:

  • Baba yake, ambaye ni gwiji wa Italia, 47, amekitumikia kikosi cha Azzurri kwenye mechi 176 na kushinda ubingwa wa Kombe la Dunia 2006 kwenye fainali zilizofanyika Ujerumani.

MILAN, ITALIA: MTOTO wa kipa mashuhuri wa Italia, Gianluigi Buffon, Louis amechagua kuitumikia Jamhuri ya Czech kwenye soka la kimataifa badala ya Azzurri, ambayo aliitumikia baba yake.

Baba yake, ambaye ni gwiji wa Italia, 47, amekitumikia kikosi cha Azzurri kwenye mechi 176 na kushinda ubingwa wa Kombe la Dunia 2006 kwenye fainali zilizofanyika Ujerumani.

Lakini, kwa Louis badala ya kufuata nyayo za baba yake, ameamua kwenda kuitumkia Jamhuri ya Czech, ambako mama yake, mrembo Alena Seredova anatokea.

Louis, 17, alianza kucheza timu ya wakubwa ya kikosi cha Pisa kwenye Serie B, alipewa nafasi ya kuchezea kwa mara ya kwanza timu hiyo mwezi uliopita chini ya kocha Filippo Inzaghi, ambaye walicheza na baba yake kwenye timu ya taifa ya Italia.

Mtoto huyo anayecheza nafasi ya winga aliitwa kuitumikia Czech kwenye kikosi cha U-18. Na kikosi chake kitamenyana na England, Ufaransa na Ureno kwenye mechi za kimataifa.

Louis alisema: "Nilifurahi sana kuja kukutana na watu tofauti na kwenye utamaduni tofauti wa soka. Nilizungumza na familia yangu na kwa pamoja tulikubaliana kwamba ni bora kwa maisha yangu ya soka kujieleza kama mchezaji nikichezea Jamhuari ya Czech.

"Mama yangu, alifurahi sana, lakini baba yangu alifurahi pia kwa sababu ilikuwa mara yangu ya kwanza kuitwa kwenye timu ya taifa."

Louis alizaliwa Turin, Italia hivyo hajui sana kuzungumza lugha ya taifa la mama yake.