Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtoko wa Liverpool Van Dijk , Salah, Trent wakiondoka utakuwaje?

MTOKO Pict

Muktasari:

  • Van Dijk ni miongoni mwa mastaa watatu matata kabisa wa Liverpool, sambamba na Mohamed Salah na Trent Alexander-Arnold, ambao mikataba yao itafika tamati mwishoni mwa msimu huu.

LIVERPOOL, ENGLAND: BAADA ya kutupwa nje na Paris Saint-Germain kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, beki wa kati na nahodha wa Liverpool, Virgil van Dijk alisema hafahamu kama ataendelea kubaki kwenye klabu hiyo hadi msimu ujao, maneno ambayo yameibua mjadala mzito.

Van Dijk ni miongoni mwa mastaa watatu matata kabisa wa Liverpool, sambamba na Mohamed Salah na Trent Alexander-Arnold, ambao mikataba yao itafika tamati mwishoni mwa msimu huu.

Van Dijk na Mo Salah kuna matumaini wanaweza kubaki, lakini kwa Trent kila kitu kinaonekana kama vile staa huyo Mwingereza anatimkia zake Real Madrid.

Lakini, muda unakimbia sana na hakuna kilichoafikiwa hadi sasa juu ya mikataba mipya ya mastaa hao, kitu ambacho kinaweza kufanya wachezaji hao watatu wote kufungasha virago vyao na kuachana na maisha ya Anfield.

Kama wataondoka bure, Liverpool itakuwa imepata hasara kubwa kuachana na wachezaji hao ambao wangeingizia pesa za kutoka klabu. Lakini, kuna swali jingine muhimu linaibuka, itakuwaje Liverpool ambayo haitakuwa na huduma ya Van Dijk, Salah na Alexander-Arnold? Kocha Arne Slot atafanya usajili gani ili kuwa na kikosi kitakachokuwa na sura mpya? Ngoja tuone kinachowezekana kutokea.

Kipa na safu ya ulinzi; Kama mastaa hao watatu wataondoka, basi eneo ambalo Liverpool haitapaswa kulipoteza pia basi ni kwa kipa Alisson golini hata kama wana mpango wa kumchukua Giorgi Mamardashvili aje kuwa Namba 1 wao mpya.

Kwenye beki wa kulia, Conor Bradley anaweza kuifanya namba hiyo kuwa yake hata kama kutakuwa na usajili mpya, huku Ibrahima Konate akitazamiwa kuwa kisiki kwenye beki ya kati kutokana na kuondoka kwa Van Dijk. Mabeki wengine, kunaweza kuwa na usajili mpya na kinachoelezwa beki wa kati wa Bournemouth, Dean Huijsen na wa kushoto Milos Kerkez wote wapo kwenye mpango.

Jarell Quansah, Andy Robertson na Joe Gomez kama hawataondoka na kubaki, basi watapata nafasi ya kucheza msimu ujao.

Safu ya kiungo; Dirisha la majira ya kiangazi 2023 lilikuwa bora kwa Liverpool na ilifanya usajili mkubwa wa kuboresha safu yao ya kiungo. Ryan Gravenberch, Alexis Mac Allister na Dominik Szoboszlai wamekuwa wachezaji muhimu kwenye eneo hilo. Lakini, kuna machaguo mengine Curtis Jones, Harvey Elliott na Wataru Endo watafanya safu hiyo kuwa imara zaidi.

Safu ya ushambuliaji; Nani ataziba pengo la Salah? Ukweli ni ngumu. Liverpool haitaweza kupata mchezaji mwingine mwenye uwezo kama wa Mo Salah wa kucheza wingi ya kulia akitumia mguu wa kushoto kwa ufasaha mkubwa. Luis Diaz amekuwa hatumiki sana upande wa kulia, kwa sababu Mo Salah yupo eneo hilo, lakini akiondoka, kocha Slot ataanza kumtumia mchezaji huyo. Federico Chiesa naye anaweza kuondoka, hivyo chaguo jingine la Liverpool kwenye safu hiyo ni la mchezaji Cody Gakpo, Diogo Jota na Darwin Nunez. Kutokana na hilo, Liverpool wanahitaji pia huduma ya straika Alexander Isak kuja kufunga mabao ili kumsahau Salah.