Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mtambue adui yako AFCON 2025

AFCON Pict

Muktasari:

  • Morocco iliyowahi kufika nusu fainali ya Kombe la Dunia 2022, ni wenyeji wa mashindano hayo huku wakiwa kati ya mataifa yanayopewa nafasi kubwa ya kunyakua ubingwa, sambamba na Nigeria, Misri, Senegal na mabingwa watetezi Ivory Coast. Mechi ya kwanza itapigwa Desemba 21 kwa wenyeji Morocco kucheza na Comoros.

RABAT, MOROCCO: MATAIFA 24 ya Afrika yatachuana kuwania ubingwa wa mashindano ya soka Afcon 2025 huko Morocco ambayo yatafanyika kwa mara ya 35.

Morocco iliyowahi kufika nusu fainali ya Kombe la Dunia 2022, ni wenyeji wa mashindano hayo huku wakiwa kati ya mataifa yanayopewa nafasi kubwa ya kunyakua ubingwa, sambamba na Nigeria, Misri, Senegal na mabingwa watetezi Ivory Coast. Mechi ya kwanza itapigwa Desemba 21 kwa wenyeji Morocco kucheza na Comoros.

Timu hizo 24 zimegawanywa kwenye makundi sita yenye timu nne kila moja, huku makala haya yakihusu uchambuzi wa kila kundi la mashindano hayo.

AFC 01

Kundi A

-Morocco

-Mali

-Zambia

-Comoros

Wenyeji Morocco ni kati ya timu imara zaidi barani Afrika na itakuwa ikitafuta taji lake la kwanza tangu 1976.

Ikiwa imeshinda mechi sita kati ya ilizocheza kwenye kufuzu na nane kati ya nane kwenye kufuzu Kombe la Dunia 2026, itakuwa kwenye Afcon 2025 ikiwa inajiamini na hasa ikiwa inacheza nyumbani.

Lakini, mambo yanaweza yasiwe rahisi kwani kundi lao lina Mali, timu inayotazamwa kama tishio kubwa kwenye michuano kutokana na ubora wao katika michuano iliyopita. Bingwa wa Afcon 2012, Zambia ikiongozwa na Patson Daka, pamoja na Comoros waliowashangaza Ghana 2022, ndio wanaokamilisha kundi hilo.

MECHI ZA KUNDI A

Desemba 21: Morocco v Comoros

Desemba 22: Mali v Zambia

Desemba 26: Morocco v Mali

Desemba 26: Zambia v Comoros

Desemba 29: Zambia v Morocco

Desemba 29: Comoros v Mali


AFC 02

Kundi B

-Misri

-Afrika Kusini

-Angola

-Zimbabwe

Misri imepangwa kwenye Kundi B ikiwa na mastaa kibao akiwamo Mohamed Salah na wachezaji wenzake wakilenga taji walilolikosa kwenye Afcon 2022. Kwenye kundi hiyo, miamba mingine ni Afrika Kusini waliorejea kwenye Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza tangu 2010, pamoja na Angola na Zimbabwe. Bafana Bafana ilifungwa nusu fainali 2024, hivyo watajaribu kwenda mbali zaidi nchini Morocco huku Lyle Foster akiwa mchezaji muhimu. Angola ilifika robo fainali mara ya mwisho, wakiongoza kundi lililomshusha Ghana hadi nafasi ya mwisho, wakati Zimbabwe wanatafuta kutinga hatua ya mtoano kwa mara ya kwanza.

MECHI ZA KUNDI B

Desemba 22: Misri v Zimbabwe

Desemba 22: Afrika Kusini v Angola

Desemba 26: Misri v Afrika Kusini

Desemba 26: Angola v Zimbabwe

Desemba 29: Angola v Misri

Desemba 29 vs Zimbabwe v Afrika Kusini


AFC 03

Kundi C

-Nigeria

-Tunisia

-Uganda

-Tanzania

Nigeria itaingia mashindanoni baada ya kushindwa kufuzu Kombe la Dunia 2026a kwa hasira zaidi kufuatia kupoteza fainali dhidi ya Ivory Coast 2024. Tunisia, iliyopita kwa kishindo kwenye kufuzu Kombe la Dunia na kupata sare ya kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Brazil ni wababe wengine wa maana kwenye kundi hilo. Kwenye karatasi, wawili hawa wanategemewa kuongoza kundi huku Uganda na Tanzania, ambayo haijashinda mechi kwa zaidi ya mwaka ikihitimisha kundi.

MECHI ZA KUNDI C

Desemba 23: Nigeria v Tanzania

Desemba 23: Tunisia v Uganda

Desemba 27: Nigeria v Tunisia

Desemba 27: Uganda v Tanzania

Desemba 30: Uganda v Nigeria

Desemba 30: Tanzania v Tunisia


AFC 04

Kundi D

-Senegal

-DR Congo

-Benin

-Botswana

DR Congo iliifunga Nigeria kwenye mchujo wa Kombe la Dunia 2026 kwenda hatua ya mtoano ya kimataifa Machi mwakani, hivyo itakwenda kwenye Afcon 2025 ikiwa na akili ya kufikiria michuano hiyo ya Marekani, Canada na Mexico.

Mbali na ushindi huo, iliitoa pia Cameroon na walikosa kufuzu moja kwa moja baada ya kupoteza 3–2 dhidi ya Senegal, ambao sasa itapata nafasi ya kulipiza. Mabingwa wa 2021, Senegal, wenye nyota wengi waliocheza Ligi Kuu England, inalenga tena ubingwa na wanajiamini baada ya kuwafunga England kwenye mechi ya kirafiki. Benin ina matumaini ya kupenya kama timu ya tatu bora, huku Botswana, ambao ni wa kiwango cha chini zaidi, wakifanya AFCON yao ya pili wakitafuta pointi ya kwanza, lakini wanaweza kushangaza kwani walitoka sare na Misri kwenye mechi za kufuzu.

MECHI ZA KUNDI D

Desemba 23: Senegal v Botswana

Desemba 23: DR Congo v Benin

Desemba 27: Senegal v DR Congo

Desemba 27: Benin v Botswana

Desemba 30: Benin v Senegal

Desemba 30: Botswana v DR Congo


AFC 05

Kundi E

-Algeria

-Burkina Faso

-Equatorial Guinea

-Sudan

Wengi wanaamini Algeria, mabingwa mara mbili, watapita kundi hili bila tabu, lakini Burkina Faso wenye Dango Ouattara wa Brentford na Bertrand Traore wa Sunderland hawatakuwa rahisi wepesi pia. Equatorial Guinea imefika hatua ya mtoano kwenye mashindano mawili yaliyopita na ikiwa na gwiji Emilio Nsue bado wakiongoza, watataka kuacha alama nyingine.

Sudan, wanaoonekana kama walioko nje ya pambano na kocha wao ni Kwesi Appiah, aliyewatoa Ghana kwa kupata pointi nne dhidi yao.

MECHI ZA KUNDI E

Desemba 24: Algeria v Sudan

Desemba 24: Burkina Faso v Equatorial Guinea

Desemba 28: Algeria v Burkina Faso

Desemba 28: Equatorial Guinea v Sudan

Desemba 31: Equatorial Guinea v Algeria

Desemba 31: Sudan v Burkina Faso


AFC 06

Kundi F

-Ivory Coast

-Cameroon

-Gabon

-Msumbiji

Ivory Coast inaendelea kuwa moja ya hadithi za ajabu za mashindano baada ya ushindi wao wa Afcon 2023 nyumbani, licha ya kukaribu kutolewa kwenye makundi na kumfukuza kocha katikati ya mashindano. Bado ni timu ngumu na wanatarajiwa kuvuka kundi bila hofu kama ile ya mara ya mwisho. Wapinzani wao wakuu watakuwa Cameroon, ambao matatizo ya ndani yanaweza kuwagharimu baada ya kumfukuza kocha Marc Brys wiki chache kabla ya mechi yao ya kwanza.

Gabon ikiongozwa na Pierre-Emerick Aubameyang, wanatazamia angalau kufika 16 bora, huku Msumbuji ikitafuta ushindi wao wa kwanza kwenye mashindano katika jaribio la sita.

MECHI ZA KUNDI F

Desemba 24: Ivory Coast v Msumbuji

Desemba 24: Cameroon v Gabon

Desemba 28: Ivory Coast v Cameroon

Desemba 28: Gabon v Msumbiji

Desemba 31: Gabon v Ivory Coast

Desemba 31: Msumbiji v Cameroon