Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

AFCON 2025: Mwali atasakwa kwenye nyasi hizi

VIWANJA Pict

Muktasari:

  • Mashindano ya Afcon 2025 yatashuhudiwa kwenye miji mitano ya Morocco, huku kila uwanja utakaotumika ukiwa na utambulisho wa kipekee kabisa, historia na ujezi wa dizaini ya kibabe kabisa inayoendana na hadhi ya mashindano hayo.

RABAT, MOROCCO: HAZIZIDI wiki mbili kabla ya kuanza kwa mchakamchaka wa mashindano ya Afcon 2025 huko Morocco na hamu ya wengi ipo kwenye viwanja venye viwango vya dunia vitakavyotumika kwenye michuano mikubwa kabisa ya soka ya kushindania ubingwa wa Afrika.

Mashindano ya Afcon 2025 yatashuhudiwa kwenye miji mitano ya Morocco, huku kila uwanja utakaotumika ukiwa na utambulisho wa kipekee kabisa, historia na ujezi wa dizaini ya kibabe kabisa inayoendana na hadhi ya mashindano hayo.

Makala haya yanaangazia viwanja vyote vitakavyotumika kwenye mashindano hayo yatakayoanza Desemba 21, 2025 hadi Januari 18, 2026.


VIWA 01

COMPLEXE SPORTIF PRINCE MOULAY

ABDELLAH

Uwezo: Mashabiki 69,500

Jiji: Rabat

Uwanja upo kilomita saba tu kutoka katikati ya jiji la Rabat na hakika Complexe Sportif Prince Moulay Abdellah ni moja ya viwanja vya soka vya hadhi ya juu vinavyopatikana Morocco. Ulizinduliwa Septemba 5, 2025 katika mechi ya kufuzu Kombe la Dunia 2026, ambapo una uwezo wa kuingiza watazamaji 68,095 huku ikielezwa utatanuliwa na kufikia watazamaji 68,700 kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia 2030. Ni uwanja wa pili kwa ukubwa huko Morocco ukifuatia baada ya Grand Stade de Tanger. Uliboreshwa 2000, 2014 na 2023 na kufikia viwango vya kimataifa.

Mechi zitakazopigwa uwanjani hapo:

-Mechi 1: Desemba 21; Morocco vs Comoros (Kundi A)

-Mechi 13: Desemba 26; Morocco vs Mali (Kundi A)

-Mechi 25: Desemba 29; Zambia vs Morocco (Kundi A)

-Mechi 39: Januari 4;

Kinara Kundi A vs wa tatu Kundi C/D/E (16 bora)

-Mechi 47: Januari 9; Mshindi 40 vs Mshindi 39 (Robo fainali)

-Mechi 50: Januari 14; Mshindi 47 vs Mshindi 46 (Nusu fainali)

-Mechi 52: Januari 18; Mshindi 49 vs Mshindi 50 (Fainali)


VIWA 02

TADE ANNEXE OLYMPIQUE COMPLEXE SPORTIF PRINCE MOULAY ABDELLAH

Uwezo: Mashabiki 21,000

Jiji: Rabat

Baadhi ya sehemu za Uwanja wa Stade Annexe Olympique Complexe Sportif Prince Moulay Abdellah zilikamilishwa ndani ya miezi tisa na ulizinduliwa Mei 25, 2025. Uwanja huo una maeneo ya kukimbia yaliyo kwenye viwanja vya kimataifa vya mita 400 huku ikiwa na sehemu ya kuchezea yenye nyasi za asili na paa lililotengenezwa katika dizaini ya kibabe kabisa. Katika uwanja huo kuna maegesho ya chini ya ardhi, vyumba vya mazoezi ya viungo, sehemu za mapumziko na studio za televisheni.

Mechi zitakazochezwa uwanjani hapo;

-Mechi 6: Desemba 23; Tunisia vs Uganda (Kundi C)

-Mechi 20: Desemba 27; Benin vs Botswana (Kundi D)

-Mechi 30: Desemba 30; Tanzania vs Tunisia (Kundi C)


VIWA 03

COMPLEXE SPORTIF PRINCE HERTITIER MOULAY EL HASSAN

Uwezo: Mashabiki 22,000

Jiji: Rabat

Umejengwa kwenye eneo la kihistoria la FUS Rabat, uwanja huo wa mjini una uwezo wa kuingiza mashabiki 22,000 wanaoketi na hauna maeneo ya kukimbilia wanariadha, hivyo unawafanya majukwaa ya mashabiki kuwa karibu kabisa na eneo la kuchezea. Mazingira ya uwanja huo ni kitu kingine kitakachokuwa na kivutio kikubwa kwa mashabiki. Uwanja huo umejengwa na kufuata ngazi tano na kuna vijumba kwa ajili ya watu maarufu wanaokwenda kutazama mechi.

Mechi zitakazochezwa uwanjani hapo;

-Mechi 9: Desemba 24; Algeria vs Sudan (Kundi E)

-Mechi 21: Desemba 28; Algeria vs Burkina Faso (Kundi E,)

-Mechi 33: Desemba 31; Equatorial Guinea vs Algeria (Kundi E)

-Mechi 43: Januari 6;  Mshindi Kundi E vs Wa pili Kundi D (16 bora)


VIWA 04

STADE EL BARID

Uwezo: Mashabiki: 18,000

Jiji: Rabat

Uwanja huo upo kwenye wilaya ya Agdal, Stade El Barid umekuwa ukitumika kama uwanja wa nyumbani wa timu ya Union Touarga SC. Una sehemu ya kuchezea ya nyasi za asili, eneo la VVIP na VIP, jukwaa la waandishi wa habari na limetengenezwa kwa kuzungukwa na maduka ya vitu kadhaa, maeneo ya kupata chakula. Uwanja huo umejengwa katika staili ya kipekee kabisa na dizaini ya sehemu ya uwanja kuingia chini kidogo ili kuwapa mashabiki fursa ya kutazama mechi kwa uhuru katika maeneo yote ya uwanja.

Mechi zitakazochezwa uwanjani hapo;

-Mechi 8: Desemba 23; DR Congo vs Benin (Kundi D)

-Mechi 18: Desemba 27; Uganda vs Tanzania (Kundi C)

-Mechi 32: Desemba 30; Botswana vs DR Congo (Kundi D)

-Mechi 40: Januari 4; Wa pili Kundi B vs Wa pili Kundi F (16 bora)


VIWA 05

STADE MOHAMMED V

Uwezo: Mashabiki 67,000

Jiji: Casablanca

Uwanja huo upo kwenye wilaya ya Maarif, Casablanca. Stade Mohammed V ni moja ya viwanja bora kabisa kwenye mchezo wa soka. Ulifunguliwa Machi 6, 1955, na ulipachipwa jina la ‘Donor’ na umeshuhudiwa ukitumika kwenye mechi nyingi hasa za mashindano makubwa. Uwanja huo una uwezo wa kuingiza mashabiki 67,000 wanaokaa na katika mashindano ya Afcon 2025 utatumika kwenye mechi nane.

Mechi zitakazochezwa katika uwanja;

-Mechi 2: Desemba 22; Mali vs Zambia (Kundi A)

-Mechi 10: Desemba 24; Burkina Faso vs Equatorial Guinea (Kundi E)

-Mechi 14: Desemba 26; Zambia vs Comoros (Kundi A)

-Mechi 22: Desemba 28; Equatorial Guinea vs Sudan (Kundi E)

-Mechi 26: Desemba 29; Comoros vs Mali (Kundi A)

-Mechi 34: Desemba 31; Sudan vs Burkina Faso (Kundi E)

-Mechi 38: Januari 3; Wa pili Kundi A vs Wa pili Kundi C (16 bora)

-Mechi 51: Januari 17;

Kusaka mshindi wa tatu


VIWA 06

GRAND STADE D’AGADIR

Uwezo: Mashabiki 45,480

Jiji: Agadir

Uwanja huo ujengwa kwenye mji wa Agadir katika eneo la pwani ya bahari ya Atlatic huko Morocco. Grand Stade d’Agadir utatumika kwenye mechi kadhaa za mashindano ya Afcon 2025. Ulizinduliwa Oktoba 11, 2013 na umejengwa katika dizaini bora kabisa inayofanya kuonekana kama moja ya nembo matata kabisa ya soka la Morocco.

Mechi zitakazochezwa uwanjani hapo;

-Mechi 3: Desemba 22; Misri vs Zimbabwe (Kundi B)

-Mechi 12: Des 24; Cameroon vs Gabon (Kundi F)

-Mechi 15: Desemba 26; Misri vs South Africa (Kundi B)

-Mechi 24: Desemba 28; Gabon vs Msumbiji (Kundi F)

-Mechi 27: Desemba 29; Angola vs Misri (Kundi B)

-Mechi 36: Desemba 31; Msumbiji vs Cameroon (Kundi F)

-Mechi 41: Januari 5; Mshindi Kundi B vs Wa tatu Kundi A/C/D (16 bora)

-Mechi 48: Januari 10; Mshindi Mechi Na.41 vs Mshindi Mechi Na.44 (Robo fainali)


VIWA 07

COMPLEXE SPORTIF DE FES

Uwezo; Mashabiki 45,000

Jiji: Fes

Complex Sportif de Fes ni uwezo wa matata kabisa uliotengenezwa kwenye eneo linalounganisha F’s na Sefrou. Kutokana na kuwa na uwezo wa kuingiza mashabiki 45,000 wanaoketi, uwanja huo umejengwa kwenye dizaini nzuri kabisa unaotoa mazingira mazuri na ya kuvutia pia kwa mashabiki wa mchezo wa soka kwa mechi za kitaifa na kimataifa. Mpango wake ulianza mwaka 1992 na ujenzi ulianza 1994 kabla ya uwanja huo kukamilika kabisa 2003.

Mechi zitakazochezwa uwanjani hapo;

-Mechi 5: Desemba 23; Nigeria vs Tanzania (Kundi C)

-Mechi  17: Desemba 27; Nigeria vs Tunisia (Kundi C)

-Mechi 29: Desemba 29; Uganda vs Nigeria (Kundi C)

-Mechi 42: Januari 5; Mshindi Kundi C vs wa tatu Kundi A/B/F (16 bora)


VIWA 08

GRAND STADE DE MARRAKECH

Uwezo: Mashabiki 45,240

Jiji: Marrakech

Uwanja huo upo kilomita 11 kaskazini kutoka katikati ya jiji. Grand Stade de Marrakech ni moja ya uwanja wa michezo uliojengwa kwenye ubora mkubwa. Ukiwa na uwezo wa kuingiza mashabiki 45,240 wanaokaa, uwanja huo umejengwa katika dizaini za kipekee kabisa ambapo unaweza kutumika kwenye mechi za mchezo wa soka na michezo mingine huku ukiwa na mzuka mkubwa kwa mashindano ya kitaifa na kimataifa. Uwanja huo pia una viti 5,000 kwenye eneo mashuhuri na eneo la ukubwa wa mita za mrada 1,000 kwa ajili ya waandishi wa habari, chumba cha utabibu na vifaa vya huduma ya kwanza.

Mechi za Afcon 2025 zitakazochezwa uwanjani hapo;

-Mechi 4: Desemba 22;

Afrika Kusini vs Angola (Kundi B)

-Mechi 11: Desemba 24; Ivory Coast vs Msumbiji (Kundi F)

-Mechi 16: Desemba 26; Angola vs Zimbabwe (Kundi B)

-Mechi 23: Desemba 28; Ivory Coast vs Cameroon (Kundi F)

-Mechi 28: Desemba 29; Zimbabwe vs Afrika Kusini (Kundi B)

-Mechi 35: Desemba 31; Gabon vs Ivory Coast (Kundi F)

-Mechi 44: Januari 6; Kinara Kundi F vs Wa Pili Kundi E (16 bora)

-Mechi 47: Januari 10; Mshindi Mechi Na.43 vs Mshindi Mechi Na.42 (Robo fainali)


VIWA 09

GRAND STADE DE TANGER

Uwezo; Mashabiki 68,000

Jiji: Tanger

Uwanja huo upo kilomita 10 kusini mwa jiji la Tangier. Grand Stade de Tanger ni uwanja wenye mvuto mkubwa kwa soka huko Morocco. Ulifunguliwa mwaka 2011 na ulipachikwa jina la Ibn Battuta, mtafiti wa karne ya 14 aliyezaliwa Tangier, jiji lililojaa utajiri mkubwa wa masuala ya kihistoria.

Mechi za Afcon 2025 zitakazochezwa uwanjani hapo;

-Mechi 7: Desemba 23; Senegal vs Botswana (Kundi D)

-Mechi 19: Desemba 27; Senegal vs DR Congo (Kundi D)

-Mechi 31: Desemba 30; Benin vs Senegal (Kundi D)

-Mechi 37: Januari 3; Winner Group D vs Third Group B/E/F (16 bora)

-Mechi 45: Januari 9; Winner Match 38 vs Winner Match 37 (Robo fainali)

-Mechi 49: Januari 14; Winner Match 45 vs Winner Match 48 (Nusu fainali)