Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Msiogope! Kuna Hincapie pale kwa Gabriel

Muktasari:

  • Mbrazili huyo alitolewa uwanjani katika mechi ya kirafiki dhidi ya Senegal iliyofanyika uwanjani Emirates wikiendi iliyopita.

LONDON, ENGLAND: BEKI wa kati wa Arsenal, Gabriel Magalhaes huenda akakaa nje ya uwanja kwa muda usiopungua wiki nne baada ya kupata maumivu ya misuli ya paja alipokuwa kwenye majukumu ya kuitumikia timu ya taifa ya Brazil.

Mbrazili huyo alitolewa uwanjani katika mechi ya kirafiki dhidi ya Senegal iliyofanyika uwanjani Emirates wikiendi iliyopita.

Na sasa kinachoripotiwa anaweza kuwa nje ya uwanja hadi Januari mwakani huku kukiwa na hofu kwamba kuna uwezekano akakosekana uwanjani kwa miezi miwili.

Gabriel atafanyiwa uchunguzi zaidi wa kuhusu maumivu hayo yanayomsumbua, lakini kwa kuanzia haonekani kama atakuwa kwenye wakati mzuri wa kucheza mechi dhidi ya Tottenham (Jumapili), Bayern Munich na Chelsea.

Na kama hilo litatokea basi beki huyo yupo kwenye hatari ya kukosa karibu mechi 15 hadi kufikia Januari katikati.

Katika kipindi ambacho beki huyo Mbrazili atakosekana uwanjani, kocha wa Arsenal, Mikel Arteta anaweza kumpa kiraka wa Ecuador, Piero Hincapie, ambaye alimsajili kwenye dirisha lililopita akitokea Bayer Leverkusen ya Ujerumani.

Gabriel amekuwa akiifanya Arsenal kuwa na beki imara sana kwenye Ligi Kuu England msimu huu, ambapo miamba hiyo ya Emirates imeruhusu mabao matano tu katika mechi 11, huku beki huyo Mbrazili akisaidia pia kuifungia mabao timu yake, akifanya hivyo mara tatu. Gabriel, 27, ni tishio kubwa kwenye mipira ya adhabu, akifunga mara mbili na kuasisti mbili pia.

Ndiye aliyekuwa mchezaji wa ndani aliyecheza dakika zote kwenye Ligi Kuu England msimu huu, huku Hincapie akiwa amecheza mechi mbili tu hadi sasa, akiwa uwanjani kwa dakika 30 tu.

Arsenal imekuwa kwenye janga la kuandamwa na majeruhi wengi, akiwamo Kai Havertz, Gabriel Jesus na Noni Madueke. Straika Viktor Gyokeres alikosa mechi iliyopita ya sare ya 2-2 dhidi ya Sunderland kabla ya mapumziko ya mechi za kimataifa, naye yupo kwenye hatihati.


MECHI ZIJAZO ZA ARSENAL

-Novemba 23 vs Tottenham (nyumbani)

-Novemba 26 vs Bayern (nyumbani)

-Novemba 30 vs Chelsea (ugenini)

-Desemba 3 vs Brentford (nyumbani)

-Desemba 6 vs Aston Villa (ugenini)