Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mourinho kubaki Uturuki, azikataa Celtic, Rangers

Mourinho Pict

Muktasari:

  • Mourinho ambaye ni mshindi mara tatu wa Ligi Kuu England akiwa na Chelsea kuelekea mchezo wao wa jana dhidi ya Rangers aliulizwa kama anaweza kufundisha moja ya timu za Scotland kati ya Celtic na Rangers na akathibitisha kwamba ana shauku ya kufanya hivyo ingawa sio kwa sasa kwani anajivunia sana kuwepo Uturuki.

ISTANBUL, UTURUKI: KOCHA wa Fenerbanhce, Jose Mourinho amekataa kuondoa uwezekano wa kwenda Rangers inayoshiriki Ligi Kuu ya Scottland.

Mourinho ambaye ni mshindi mara tatu wa Ligi Kuu England akiwa na Chelsea kuelekea mchezo wao wa jana dhidi ya Rangers aliulizwa kama anaweza kufundisha moja ya timu za Scotland kati ya Celtic na Rangers na akathibitisha kwamba ana shauku ya kufanya hivyo ingawa sio kwa sasa kwani anajivunia sana kuwepo Uturuki.

Mbwatukaji huyo aliongeza kwamba kazi ya ukocha inahitaji uaminifu lakini angezingatia nafasi hiyo huko baadaye.

"Inawezekana katika siku zijazo, lakini kwa sasa sitafuti kazi mpya."

Hata hivyo, kocha huyu ambaye ni mshindi mara mbili wa Ligi ya Mabingwa hii si mara ya kwanza kuhusishwa na mpango wa kurudi Uingereza tangu atue Uturuki.

Mnamo Oktoba 2024, Mourinho alitoa tamko kwamba anaweza kwenda England kuifundisha Everton iliyokuwa katika hatihati ya kuachana na Sean Dyche.

Baadaye alisema tamko hilo lilikuwa ni mzaha tu ingawa mashabiki wengi wamekuwa wakitamani kuona akirejea Uingereza.

"Ni ligi iliyochangamka. Kwangu ni kila kitu ninachopenda, kinachagizwa na amsha amsha, kucheza kwenye viwanja vilivyo tupu kwangu haifai. Celtic na Rangers… ni timu kubwa na mashabiki wakubwa na hisia kubwa, majukumu makubwa, matarajio makubwa," alisema Mourinho kuhusu uwezekano wa kutua Scottland.