Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Morocco kupinga adhabu ya CAF, yaundaa kamati maalum kujadili

MOROCCO Pict

Muktasari:

  • Uamuzi huo umekuja kufuatia kipigo cha Morocco cha bao 1–0 dhidi ya Senegal katika mechi ya fainali iliyopigwa jijini Rabat Januari 18, 2026 ambapo Senegal iliibuka kidedea baada ya muda wa ziada.

SHIRIKISHO la Soka la Kifalme la Morocco (FRMF) limetangaza litakata rufaa kupinga hatua za kinidhamu zilizochukuliwa baada ya fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025).

Uamuzi huo umekuja kufuatia kipigo cha Morocco cha bao 1–0 dhidi ya Senegal katika mechi ya fainali iliyopigwa jijini Rabat Januari 18, 2026 ambapo Senegal iliibuka kidedea baada ya muda wa ziada.

Katika taarifa iliyotolewa kupitia kikao cha Alhamisi, Februari 26, 2026 shirikisho hilo liliweka wazi mpango wake wa kuitisha kikao maalum cha kutathmini matukio yote yaliyohusiana na fainali hiyo pamoja na adhabu zilizotolewa na Shirikisho la Soka la Afrika (CAF).

Hoja Kuu ambazo zitapitiwa na kikao maalum cha kutathmini matukio hayo:

Adhabu Zilizopitiliza: Viongozi wa Morocco wanadai kuwa adhabu walizopewa wachezaji na timu yao ni kali mno ikilinganishwa na makosa yaliyofanyika.

Upendeleo kwa Senegal: Shirikisho hilo linahoji kuwa adhabu zilizotolewa upande wa Senegal hazilingani na uzito wa matukio yaliyotokea uwanjani.

Haki na Uwazi: 
Morocco imeutaja uamuzi wa Kamati ya Nidhamu ya CAF haukikidho haki na imesisitiza kuwa itatumia taratibu zote za kisheria kupata haki.

"Kikao maalum kitafanyika kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) siku zijazo," imeeleza taarifa hiyo, huku ikibainisha kuwa mchakato wa kisheria kuhusu fainali hiyo tayari umeanza.

Shirikisho hilo limesisitiza kuwa hatua hiyo ya kukata rufaa inalenga kulinda heshima ya kanuni za soka na kuhakikisha uwepo wa mchakato wa kinidhamu ulio sawa na wa wazi.

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) lilitangaza adhabu kwa mataifa ya Senegal na Morocco kufuatia vurugu na utovu wa nidhamu zilizojitokeza wakati wa mechi ya fainali ya AFCON 2025 iliyofanyika Januari 18, 2026. 


Adhabu kwa Senegal (Mabingwa)
Pape Thiaw (Kocha Mkuu): Amefungiwa mechi tano (5) za CAF na kupigwa faini ya $100,000 (Sh258 milioni) kwa kuchochea wachezaji kutoka nje ya uwanja kupinga maamuzi ya mwamuzi.


Wachezaji: Iliman Ndiaye na Ismaila Sarr wamefungiwa mechi mbili (2) kila mmoja kwa utovu wa nidhamu dhidi ya mwamuzi.

Faini ya Shirikisho la Senegal (FSF): Jumla ya faini ni $615,000 (Sh 1.6 bilioni), ikijumuisha $300,000 (Sh780 milioni) kwa vurugu za mashabiki na $300,000 (Sh780 milioni) nyingine kwa utovu wa nidhamu wa wachezaji na benchi la ufundi. 


Adhabu kwa Morocco (Wenyeji)
Achraf Hakimi: Amefungiwa mechi mbili (2), ambapo mechi moja ataitumikia mara moja na nyingine itakuwa ya uangalizi kwa mwaka mmoja.

Ismaël Saibari: Amefungiwa mechi tatu (3) na kupigwa faini ya $100,000 (Sh258 milioni).

Faini ya Shirikisho la Morocco (FRMF): Jumla ya faini ni $315,000 (Sh819 milioni). Hii inajumuisha $200,000 (Sh520 milioni) kwa tabia mbaya ya 'ball boys' na $100,000 (Sh258 milioni) kwa wachezaji na viongozi kuingia eneo la VAR na kumsumbua mwamuzi.

Mashabiki: Faini ya $15,000 (Sh39 milioni) kwa matumizi ya mionzi ya "laser" wakati wa mechi.