Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kamati ya utendaji RMFF kuamua mrithi wa Walid Regragui

MOROCCO Pict

Muktasari:

  • Benchi la ufundi la timu ya taifa ya Morocco linaongozwa na kocha Walid Regragui ambaye anatarajiwa kujadiliwa kwenye kikosi hicho, baada ya kuwasilisha barua ya kujiuzulu kufuatia kushindwa kwenye mechi ya fainali ya AFCON 2025.

KAMATI ya Utendaji ya Shirikisho la Soka la Morocco (RMFF), inatarajia kukutana leo Alhamisi ili kuamua mustakabali wa benchi la ufundi la timu ya taifa hilo ambalo mara ya mwisho lilipoteza mechi ya fainali ya AFCON 2025 dhidi ya Senegal.

Benchi la ufundi la timu ya taifa ya Morocco linaongozwa na kocha Walid Regragui ambaye anatarajiwa kujadiliwa kwenye kikosi hicho, baada ya kuwasilisha barua ya kujiuzulu kufuatia kushindwa kwenye mechi ya fainali ya AFCON 2025.

Awali uongozi wa RMFF, uliripotiwa kuikataa barua ya ombi la kujiuzulu kwa kocha huyo, lakini baadaye ikaelezwa itawasilishwa mbele ya kamati ya utendaji kwa ajili ya kujadiliwa na kuamuliwa kuondoka ama kubaki.

Jarida la Ufaransa Foot Mercato limeripoti kuwa, tamko la awali la RMFF limeanza mchakato wa kusaka kocha mpya, na huenda kikao cha leo kikaidhinisha mrithi wa Regragui, kabla ya mechi za kimataifa za kirafiki Machi mwaka huu.

Taarifa za kipekee kutoka Foot Mercato zinaonyesha kuwa, Mohamed Wahbi anatarajiwa kuchukua nafasi ya kocha mkuu wa timu ya taifa ya Morocco katika kipindi hiki cha kuelekea Kombe la Dunia 2026. 

Wahbi ana uzoefu mkubwa wa maendeleo ya vijana, baada ya kuiongoza timu ya taifa ya miaka 17 akifanya kazi katika timu za vijana za R.S.C. Anderlecht kabla ya kuteuliwa na RMFF Machi 2022 kuiongoza timu ya taifa chini ya miaka 20.

Chini ya uongozi wake, timu za vijana za Morocco zimepiga hatua kubwa. Akifanya vizuri kufikia fainali ya AFCON U20 na kufanikisha historia kwa kushinda taji la Kombe la Dunia la U20 Oktoba 2025 nchini Chile, ikiwa ni ushindi wa kwanza wa kimataifa kwa taifa hilo la Afrika magharibi.

Shirikisho la Soka la Morocco limezingatia wagombea wengine maarufu, ikiwa ni pamoja na kocha wa zamani wa FC Barcelona, Xavi Hernandez, Tarik Sektioui, aliyeiwezesha Morocco kushinda kombe la ubingwa wa nchi za kirabu na kupata nafasi ya tatu katika michuano ya Olympiki.