Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Morocco yashinikizwa kuwaachia waliohukumiwa AFCON 2025

SENEGAL Pict

Muktasari:

  • Mashabiki hao walikamatwa na kuhukumiwa kufuatia ghasia zilizozuka wakati wa mechi ya fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) mwezi Januari 2026, ambapo Senegal iliibuka bingwa kwa kuifunga Morocco bao 1-0.

MAMIA ya wananchi nchini Senegal, wameingia mitaani katika Jiji la Dakar kwa lengo la kuishinikiza Serikali ya Morocco kuwaachia huru mashabiki 18 wa soka wa nchi hiyo wanaotumikia vifungo gerezani nchini humo.

Mashabiki hao walikamatwa na kuhukumiwa kufuatia ghasia zilizozuka wakati wa mechi ya fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) mwezi Januari 2026, ambapo Senegal iliibuka bingwa kwa kuifunga Morocco bao 1-0.

Februari 19, 2026 mahakama moja jijini Rabat, Morocco, iliwahukumu mashabiki hao kifungo cha kati ya miezi mitatu hadi mwaka mmoja kwa kosa la kufanya fujo uwanjani. Mashabiki tisa miongoni mwao walihukumiwa kifungo cha juu cha mwaka mmoja pamoja na faini ya Euro 460 (Sh1.4 milioni).

Ghasia hizo ziliripotiwa kuanza mwishoni mwa mchezo wa fainali baada ya mwamuzi kuipa Morocco mkwaju wa penalti. Baadhi ya mashabiki wa Senegal walijaribu kuvunja uzio wa usalama na kuingia uwanjani, jambo lililozua makabiliano makali na maafisa usalama wa Morocco.

Waziri Mkuu wa Senegal, Ousmane Sonko, akizungumza bungeni, alikosoa hukumu hiyo na kusema kuwa hatua iliyochukuliwa na Morocco inaweza kuharibu uhusiano wa kidiplomasia kati ya mataifa hayo mawili rafiki.

"Serikali ya Senegal inafanya kila linalowezekana kuhakikisha raia wetu wanarejea nyumbani salama," amesema Sonko, akisisitiza kuwa hukumu hiyo ni kali mno ikilinganishwa na mazingira ya soka.

Licha ya mvutano huo wa kisheria, Senegal inaendelea kusherehekea ubingwa wa AFCON 2025 baada ya mshambuliaji wa Morocco, Brahim Diaz, kukosa penalti muhimu katika muda wa nyongeza, jambo lililoipa Senegal taji la Afrika kwa mara nyingine.

Hadi sasa, waandamanaji nchini Senegal wameapa kuendelea na shinikizo hilo hadi hapo ndugu zao watakaporudishwa nyumbani, huku kukiwa na matumaini ya kuingiliwa kati kwa mazungumzo ya ngazi za juu kati ya Senegal na Morocco.