Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mo Salah mchezaji bora wa mwaka

MO SALAH Pict

Muktasari:

  • Salah, 32, anakuwa mchezaji wa pili kushinda tuzo hiyo mara tatu na kulingana na gwiji wa Arsenal, Thierry Henry.

LIVERPOOL, ENGLAND: SUPASTAA wa Liverpool, Mohamed Salah amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka wa Chama cha Waandishi wa Habari huko England baada ya staa huyo wa Misri kupigiwa kura zaidi ya asilimia 90.

Salah, 32, anakuwa mchezaji wa pili kushinda tuzo hiyo mara tatu na kulingana na gwiji wa Arsenal, Thierry Henry.

Straika wa Arsenal, Alessia Russo naye amechaguliwa kuwa Mchezaji Bora wa Mwaka kwa upande wa wanawake baada ya mchuano mkali, lakini hatimaye ni yeye aliyeibuka kuwa mshindi.

Salah, 32, amekuwa na mchango mkubwa kwenye ubingwa wa Liverpool wa Ligi Kuu England msimu huu, akivunja rekodi mbalimbali za mabao. Staa huyo alisaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki Liverpool hivi karibuni, akiongeza miaka miwili, amefunga mabao 28 kwenye Ligi Kuu England. Salah ameweka jina lake kwenye vitabu vya kumbukumbu kubwa Anfield na kutajwa kama mmoja wa magwiji wa muda wote katika zama za Ligi Kuu England. Mchezaji mwenzake wa Liverpool, Virgil van Dijk ndiye aliyekuwa mshindani wake baada ya beki huyo wa kati wa Kidachi kumaliza katika nafasi ya pili kwenye zoezi ya kupigiwa kura.

Beki Van Dijk naye alikuwa na mchango mkubwa wa ubingwa huo wa Liverpool na kumsaidia kocha Arne Slot kubeba taji la Ligi Kuu England katika msimu wake wa kwanza. Straika wa Newcastle United, Alexander Isak alishika nafasi ya tatu na kiungo ghali wa Arsenal, Declan Rice alishika namba nne. Isak aliisaidia Newcastle kushinda taji kwa mara ya kwanza baada ya miaka 56 iliponyakua ubingwa wa Kombe la Ligi.

Rice alikuwa silaha muhimu ya Arsenal kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya, alifunga kwa friikiki mbili dhidi ya Real Madrid uwanjani Emirates kumbukumbu itakayobaki milele. Nje ya Top Four, kulikuwa na mastaa wengine 15 waliopigiwa kura 918 za wajumbe.