Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mnigeria apanga kujiondoa Wolverhampton Wanderers

MNIGERIA Pict

Muktasari:

  • Wolves imeshuka Ligi Kuu England tangu ilipopanda 2018 kipindi ambacho ilimaliza nafasi ya saba mara mbili na kufika robo fainali ya Europa League 2019/20. Wolves inaikaribisha Tottenham Hotspur na Sunderland mechi mbili zijazo.

WOLVERHAMPTON, ENGLAND: NYOTA wa kimataifa wa Nigeria, Tolu Arokodare anatarajia kuondoka Wolverhampton Wanderers dirisha lijalo la usajili kufuatia ugomvi uliotokea ndani ya chumba cha kubadilishia nguo.

Arokodare mwenye thamani ya Pauni 23 milioni anatarajiwa kuondoka baada ya kuwa chanzo cha ugomvi chumbani, ambapo aligombana na mchezaji mwenzake, Mateus Mane, baada ya timu yao kufungwa na West Ham United mapema mwezi huu.

Inaelezwa kuwa Arokodare ndiye aliyekuwa chanzo cha mtifuano huo baada ya kichapo cha mabao 4-0 katika Uwanja wa London Stadium, Aprili 10, matokeo yaliyochochea zaidi timu hiyo kuwa hatarini kushuka daraja. Arokodare aliingia uwanjani kwa dakika 19 tu katika mechi hiyo.

Katika mechi iliyofuata, alipokuwa benchi bila kutumika wakati Wolves walifungwa 3-0 na Leeds United, ilionekana wazi kuwa nafasi yake ndani ya kikosi inapungua licha ya kuwa bado ana mkataba wa miaka minne. Mchezaji huyo mwenye miaka 25 alinunuliwa kutoka RC Genk kwa Pauni  23 milioni msimu uliopita akisaini hadi 2029, huku akiwa na chaguo la kuongeza mwaka mmoja zaidi.

Vyanzo kutoka ndani ya klabu vinasema suala hilo la ugomvi tayari limeshughulikiwa, lakini inaonekana hatakuwa sehemu ya kikosi cha Wolves kitakachocheza Championship msimu ujao. Arokodare amefunga mabao matatu katika mechi 28 za ligi msimu huu, bao lake la mwisho likiwa katika sare ya mabao 2-2 dhidi ya Brentford, mwezi Machi 16.

Kwa sasa, kikosi hicho cha kocha Rob Edwards kimeshuka daraja baada ya kupoteza mechi mbili mfululizo. Wolves ina pointi 15. Kushuka kwao kumechochewa na suluhu kati ya West Ham United na Crystal Palace.

Wolves imeshuka Ligi Kuu England tangu ilipopanda 2018 kipindi ambacho ilimaliza nafasi ya saba mara mbili na kufika robo fainali ya Europa League 2019/20. Wolves inaikaribisha Tottenham Hotspur na Sunderland mechi mbili zijazo.