Wolves yashuka daraja, kucheza Championship msimu ujao
Muktasari:
- Matokeo hayo yameifanya Wolves kushuka daraja moja kwa moja kwani haitoweza kuzifikia pointi ilizo nazo West Ham kwa sasa na ikiwa imebakiza mechi tano.
Suluhu ya bila kufungana kati ya Crystal Palace dhidi ya West Ham kumeifanya timu ya Wolves kushukuka daraja, itacheza Championship msimu ujao 2026/27.
Matokeo hayo yameifanya Wolves kushuka daraja moja kwa moja kwani haitoweza kuzifikia pointi ilizo nazo West Ham kwa sasa na ikiwa imebakiza mechi tano.
Kwa sasa Wolves inapointi 17 katika mechi 33 ilizocheza na hata ikishinda mechi zote tano zilizobaki itafikisha pointi 32 pungufu ya pointi 1 ya pointi ilizonazo West Ham kwa sasa, ikiwa na pointi 33 kwenye mechi 33 ilizocheza.
Kupitia ukitaka rasmi wa instagram wa klabu hiyo, Mwenyekiti wa klabu hiyo Nathan Shi amechapisha ujumbe ulionyeshwa kusikitishwa na taarifa hizo na kuonyesha mikakati waliyoipata nayo kwa sasa ya kuijenga timu na kurejea kwa nguvu EPL.
“Kuthibitishwa kwa kushushwa daraja kwetu ni wakati mgumu kwa kila mtu aliyeunganishwa na Wolves. Ingawa hii ni matokeo ya kukatisha tamaa sana, kazi imekuwa ikiendelea tangu nilipofika Desemba ili kuhakikisha tuko tayari kujibu kwa uwazi na imani”.
“Tunaelewa kinachohitaji kuboreshwa, na lengo letu sasa ni kuimarisha klabu, kujenga kasi na kuunda timu ambayo mashabiki wetu wanaweza kuamini. Tunajua kinachohitajika na tutakaribia miezi ijayo kwa kusudi”.
“Tunajua msimu huu umejaribu uaminifu na uvumilivu wako. Uungaji mkono wako, nyumbani na ugenini, haujachukuliwa kirahisi. Unastahili bora zaidi, na kukupa klabu unayoweza kujivunia kwa dhati ndio kinachoendesha kila kitu tunachofanya kuanzia sasa”
Wakati Wolves ikishika daraja, Coventry City ya Frank Lampard yenyewe imepanda daraja na itacheza EPL msimu ujao.
Timu zingine zilizopo kwenye hati hati ya Mishima daraja ni Tottenham Hotspurs iliyopo nafasi ya 18 na pointi 31, na Burnley iliyopo nafasi ya 19 ikiwa na pointi 20.