Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

De Zebri awatoa 'OUT' mastaa Spurs kuwaokoa kushuka daraja

EPL Pict

Muktasari:

  • Kwa mujibu wa taarifa, De Zerbi aliandaa chakula hicho katika mgahawa maarufu wa kifahari wa Mayfair, Bacchanalia, baada ya kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Sunderland, ambayo ilikuwa mechi yake ya kwanza kukinoa kikosi hicho.

LONDON, ENGLAND: KOCHA wa Tottenham Hotspur, Roberto De Zerbi ameibua mjadala baada ya kuwapeleka wachezaji wake katika mgahawa wa kifahari jijini London, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuinua morali ya kikosi hicho kinachopambana kuepuka kushuka daraja.

Hatua hiyo imekuja wiki chache baada ya mtangulizi wake, Igor Tudor, kushindwa kuisaidia timu hiyo kujinasua na matokeo mabaya licha ya kufanya tukio kama hilo wakati wa kipindi chake kifupi cha kuinoa Spurs.

Mashabiki wa Tottenham hawakufurahishwa na uamuzi huo, wakikosoa na kueleza historia inaonyesha mbinu hiyo haikusaidia kwani baada ya tukio la Tudor, timu ilipoteza mechi mbili mfululizo kabla ya kocha huyo kuondolewa.

EP 01

Kwa mujibu wa taarifa, De Zerbi aliandaa chakula hicho katika mgahawa maarufu wa kifahari wa Mayfair, Bacchanalia, baada ya kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Sunderland, ambayo ilikuwa mechi yake ya kwanza kukinoa kikosi hicho.

Kwa sasa, Tottenham inashika nafasi ya 18 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England ikiwa na pointi 30, baada ya kushinda mechi saba, sare tisa na kupoteza 16, hali inayowaweka katika hatari kubwa ya kushuka daraja kwa mara ya kwanza baada ya zaidi ya miaka 90.

Akijitetea, De Zerbi amesema jukumu lake kubwa kwa sasa si kufundisha mbinu bali kurejesha hali ya kujiamini kwa wachezaji wake.

EP 02

“Kazi yangu sasa siyo kufundisha mbinu za kucheza, bali kuwapa wachezaji kile wanachohitaji kisaikolojia,” amesema De Zerbi.

Mgahawa huo wa Bacchanalia unajulikana kwa mazingira ya kifahari na huduma za hali ya juu, ukiwavutia watu mashuhuri mbalimbali duniani. Bei zake pia ziko juu na sahani moja inaweza kugharimu kati ya Pauni 34 hadi 135.

Katika hali ya sasa, Spurs haijashinda mechi yoyote ya Ligi Kuu England tangu mwanzo wa mwaka, huku kipigo cha hivi karibuni kikizidi kuwavuta kwenye mstari wa kushuka daraja.

EP 03

Awali, Tudor aliwahi kuandaa chakula cha pamoja kabla ya dabi ya Kaskazini mwa London dhidi ya Arsenal Februari 22 na  Spurs ilichapwa mabao 4-1, na baadaye kuondolewa madarakani baada ya siku 44 tu kutokana na matokeo mabaya.

Licha ya changamoto hizo, De Zerbi anaripotiwa kuanza kujenga uhusiano mzuri na wachezaji, tofauti na Tudor ambaye alikosolewa kutokana na ukali wake.

EP 04

Habari njema kwa Spurs ni kurejea mazoezini kwa kiungo Rodrigo Bentancur, aliyekuwa nje tangu Januari kutokana na jeraha la misuli ya paja. Hata hivyo, nahodha Cristian Romero ameondolewa hadi mwisho wa msimu kutokana na jeraha la goti.

Tottenham inatarajia kushuka dimbani leo dhidi ya Brighton kabla ya kukutana na Aston Villa na Chelsea katika michezo ya mwisho ya msimu.

EP 05

MECHI ZINAZOPIGWA LEO LIGI KUU ENGLAND

Brentford v Fulham (saa 6:30 mchana)

Leeds Uitd v Wolves (saa 9:00 alasiri)

Newcastle United v Bournemouth (saa 9:00 alasiri)

Spurs v Brighton (saa 11:30 jioni)

Chelsea v Man United (saa 2:00 usiku)