Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Misri, Sauzi zapenya Dube akiaga Afcon 2025

ZIMEFUZU Pict

Muktasari:

  • Kwenye dakika ya 19, mshambuliaji huyo wa Motherwell aliwapiga chenga mabeki kadhaa wa Afrika Kusini kabla ya kuusukumia mpira nyavuni akiandika bao la kusawazisha kwa Zimbabwe na ubao kusomeka 1-1.

RABAT, MOROCCO: TAWANDA Maswanhise amefunga bao matata kabisa wakati Zimbabwe ikichapwa 3-2 na Afrika Kusini na hivyo kutupwa nje ya mashindano ya Afcon 2025 yanayoendelea huko Morocco.

Kwenye dakika ya 19, mshambuliaji huyo wa Motherwell aliwapiga chenga mabeki kadhaa wa Afrika Kusini kabla ya kuusukumia mpira nyavuni akiandika bao la kusawazisha kwa Zimbabwe na ubao kusomeka 1-1.

Afrika Kusini ilitangulia kufunga kwa bao la dakika ya saba lililowekwa kimiani na Tshepang Moremi.

Kwa kipindi cha kwanza hakukuwa na mabao mengine, hadi hapo mapema kwenye kipindi cha pili, Bafana Bafana ilipofunga tena kupitia kwa Lyle Foster, lakini Zimbabwe ilisawazisha baada ya Aubrey Modiba kujifunga.

Wakati mambo yakionekana kama Zimbabwe inakwenda kupata pointi yake ya pili kwenye Kundi B la mashindano hayo ya Afcon 2025, mambo yalitibuka baada ya kusababisha penalti, iliyowekwa kwenye nyavu na Oswin Appollis na hivyo, Afrika Kusini kushinda 3-2, matokeo yanayowafanya kufikisha pointi sita na kuungana na Misri katika mtoano.

Katika mchezo mwingine wa kundi hilo, Misri iliyowapumzisha mastaa wake muhimu, Mohamed Salah na Omar Marmoush ilitoka sare ya bila kufungana na Angola, huku ikisonga hatua ya 16 bora kutokana na kufikisha pointi saba.

Mabingwa hao mara saba wa Afrika, Misri tayari ilikuwa imeshafuzu mtoano, hivyo katika mechi hiyo ya kukamilisha ratiba iliichezesha kikosi tofauti kabisa na hivyo kufanikiwa kupata sare.

Angola imemaliza hatua ya makundi ikiwa na pointi mbili kwenye nafasi ya tatu, huku Zimbabwe ya Prince Dube ikikusanya virago na kutupwa nje.

Misri itaendelea kubaki mjini Agadir ikisubiri mpinzani wa kwenye mechi ya hatua ya 16 bora, ambapo inaweza kuwa timu itakayovuka kwa mtindo ya tatu bora kutoka kwenye Kundi A, C au D.