Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Milio ya risasi yaahairisha mechi ya Hockey

Magongo Pict
Magongo Pict

Muktasari:

  • Kipande cha video kilichorekodiwa katika tukio hilo kilionyesha wachezaji kutoka Chuo Kikuu cha St. Louis na La Salle wakiacha vifaa vyao na kukimbilia ndani ya vyumba, huku ofisa mmoja akionekana kuteleza kabla ya kuinuka kuendelea kukimbia.

MECHI ya hockey iliyochezwa Philadelphia, ililazimika kusimamishwa na wachezaji kukimbilia vyumbani baada ya milio ya risasi kusikika uwanjani.

Kipande cha video kilichorekodiwa katika tukio hilo kilionyesha wachezaji kutoka Chuo Kikuu cha St. Louis na La Salle wakiacha vifaa vyao na kukimbilia ndani ya vyumba, huku ofisa mmoja akionekana kuteleza kabla ya kuinuka kuendelea kukimbia.

Baada ya tukio hilo, taarifa katika ukurasa wa X wa Chuo Kikuu cha St. Louis ulieleza kwamba hakukuwa na mtu aliyedhurika katika tukio hilo.

“Mechi ya leo dhidi ya La Salle imeiahirishwa kwa sababu ya milio ya bunduki iliyoibuka, lakini kila mtu yupo salama.’’

Msemaji wa Chuo Kikuu cha St. Louis alikataa kutoa maelezo yoyote ya ziada alipowasiliana na tovuti ya DailyMail.com. Hata hivyo, polisi wa Philadelphia walisema ufyatuaji risasi ulifanyika katika maegesho ya karibu yaliyokuwa kwenye uwanja huo.

“Mhalifu alikuwa akipiga risasi kutokea maegesho. Hata hivyo alikimbia kutoka eneo la tukio kabla ya polisi kufika. Hakuna majeruhi waliopatikana,” ilisema taarifa ya polisi wa eneo hilo.

“Baada ya hapo eneo la tukio lililindwa hakuna mtu aliyekamatwa wala silaha iliyopatikana. Mhalifu anadaiwa kuwa ni mwanaume mweusi aliyevalia kofia nyeusi, uchunguzi bado unaendelea.”