Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mikel Arteta: Sikumaanisha hivyo, sina ugomvi na Guradiola

Muktasari:

  • Arteta alichafua hali ya hewa alipotoa kauli anajua kinachoendelea Man City na kusababisha kutupiana maneno kuanzia makocha hadi wachezaji, kabla ya kocha huyo msaidizi wa Guardiola kukubali yaishe kwa kudai hana ugomvi na bosi wake huyo wa zamani na anamheshimu sana yeye na wafanyakazi wa Man City.

LONDON, ENGLAND: BAADA ya joto la majibizano kuzidi kupanda kwa makocha wa Manchester City na wa Arsenal, hali imetulia kwa miamba hiyo inayotajwa kuwa na ushindani mkubwa msimu huu kwenye Ligi Kuu England na Mikel Arteta amesema hakuwa na maana nyingine na alichokisema juu ya City na hana ugomvi na Pep Guardiola.

Arteta alichafua hali ya hewa alipotoa kauli anajua kinachoendelea Man City na kusababisha kutupiana maneno kuanzia makocha hadi wachezaji, kabla ya kocha huyo msaidizi wa Guardiola kukubali yaishe kwa kudai hana ugomvi na bosi wake huyo wa zamani na anamheshimu sana yeye na wafanyakazi wa Man City.

Arteta aliyeiongoza Arsenal kwenye ushindi wao wa nne msimu huu dhidi ya Leicester juzi Jumamosi, aliingia kwenye majibizano ya vijembe na Guardiola baada ya mchezo wao wa sare ya mabao 2-2 wa Ligi Kuu England, Septemba 22, kwenye dimba la Etihad.

Wachezaji wa Man City waliiponda Arsenal inacheza mchezo mchafu kwa kujidondosha ovyo ili kupoteza muda na kwenye mchezo huo wa sare walifanya hivyo na kupata sare ugenini Etihad.

Siku kadhaa baada ya kauli hizo, Arteta akiwa katika mkutano na waandishi wa habari kabla ya mchezo wao wa Carabao dhidi ya Bolton, alisema kauli hizo za kusaka sare sio za kweli na kuongeza ana taarifa zote juu ya kile kinachoendelea ndani ya Man City.

Baada ya kauli hiyo, kwenye mkutano na wanahabari Ijumaa kabla ya mchezo dhidi ya Newcastle United, Guardiola alimtaka Arteta afafanue kuhusu kauli yake ya anajua nini kuhusu Man City.

"Wakati ujao Mikel anapaswa kuwa wazi zaidi kuhusu anachomaanisha, kuhusu kuwa hapa kwa miaka minne na kujua nini hasa kinachoendelea. Kwa sababu inaweza ikahusu mchakato uliosabaisha tuwe na mashtaka 115. Anaweza kuwa na habari," alisema Guardiola.

Akijibu kile alichokisema bosi wake wa zamani, Arteta alisema: "Narudia ili nieleweke vizuri sana. Nampenda Pep."

"Nimekuwa nikimpenda tangu nikiwa na umri wa miaka 10. Ninamheshimu sana na ninashukuru sana kwa chochote alichonifanyia na anachoendelea kunifanyia.

"Namwona kuwa rafiki. Ninampenda na kumheshimu kila mfanyakazi pale (City) kwa sababu nilifanya nao kazi kwa miaka minne."

"Ninaposema 'ninawajua', nilimaanisha najua jinsi wanavyofanya kazi kwa bidii," alisema Arteta. "Sijaona binadamu akifanya kazi kwa bidii kama Pep, wasaidizi wake na kila mtu katika timu yao. Sababu ya wao kuwa imara siku zote ni hali hiyo ya kufanya kazi sana na kuwa na njaa ya mafanikio. Hivi ndivyo nilivyojifunza na nilichomaanisha, sidhani kama nina maelezo zaidi ya hayo," aliongeza Arteta.

"Ukitaka naweza kurudia maelezo yangu lakini kama mtu anataka kuharibu uhusiano wetu, hilo halipo mikononi mwangu, lakini bado nina uhusiano na watu wote kwenye timu hiyo."

Arsenal kwa sasa inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 14 ilizokusanya kwenye mechi sita za EPL.