Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mchumba wa Diaz aaga Liverpool

DIAZ Pict

Muktasari:

  • Diaz amekuwa kipenzi cha mashabiki wa Liverpool katika misimu minne iliyopita, lakini staa huyo wa Colombia ameendelea kuhusishwa kuwa anaweza kuondoka dirisha lijalo la  majira ya kiangazi, huku Barcelona na Al-Nassr zikihusishwa naye.

LIVERPOOL, ENGLAND: MCHUMBA wa Luiz Diaz ambaye ni mshambuliaji wa Liverpool, Gera Ponce amechapisha ujumbe wa hisia kwenda kwa mashabiki wa Liverpool ambao unahisiwa kuwa ni miongoni mwa nyota walio mbioni kuondoka.

Diaz amekuwa kipenzi cha mashabiki wa Liverpool katika misimu minne iliyopita, lakini staa huyo wa Colombia ameendelea kuhusishwa kuwa anaweza kuondoka dirisha lijalo la  majira ya kiangazi, huku Barcelona na Al-Nassr zikihusishwa naye.

Gera ameongeza uvumi kwa kuandika ujumbe wa kuushukuru mji wa Liverpool  na mashabiki kupitia mitandao ya kijamii jambo ambalo lilionyesha kuwa huenda Diaz asiwepo Anfiled msimu ujao. Kupitia Instagram, aliposti picha kutoka mechi ya mwisho ya nyumbani msimu huu: “Kwa mashabiki wa kipekee wa Liverpool, tangu siku ya kwanza tulipowasili tulihisi moja kwa moja maana ya kuwa sehemu ya timu hii. Tulijua kaulimbiu ni ‘You’ll Never Walk Alone’, lakini kuwasikia mkiimba kwa hisia kubwa, kutoa sapoti kila wakati na kuonyesha upendo wa dhati kulituthibitishia hapa huwezi kutembea peke yako.

“Asanteni kwa upendo mwingi, kwa kujitolea na kutufanya tuhisi tuko nyumbani. Kuwa sehemu ya mashabiki hawa ni heshima. Bila shaka yoyote nyinyi ni bora zaidi duniani.

“Huu ni uhusiano wa kweli, wa kina na wenye nguvu unaothibitisha kwamba hatutatembea peke yetu kamwe.”

Baada ya ujumbe baadhi ya mashabiki wa Liverpool waliandika kwenye mtandao wa X (zamani Twitter), ambapo mmoja aliandika: “Ni wazi ataondoka majira haya ya kiangazi.” Mwingine aliongeza “Hii inaonekama kama tunaagwa.” Akaunti moja ya LFCApproved iliandika: “Nadhani ni haki kusema Diaz anaondoka baada ya yeye na mke wake kuposti ujumbe wa kuaga kwenye mitandao ya kijamii.”

Ingawa hakuna tangazo rasmi ujumbe huo umetafsiriwa kama dalili kuwa safari ya Diaz imefika.