Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbrazili wa Real Madrid afunguka mazito

MBRAZIL Pict

Muktasari:

  • Beki huyo wa kulia wa zamani wa Brazil, Cicinho, aliichezea Real Madrid kwa miezi 18 kabla ya kwenda kujiunga na AS Roma ya Italia, Agosti 2007.

MADRID, HISPANIA: KUISHI kwingi, kuona mengi. Ndicho unachoweza kusema baada ya mchezaji Cicinho kuibuka na kufichua kwamba alikuwa akinywa bia 10 kwa siku na alikuwa akienda mazoezini kwenye kikosi chake cha Real Madrid akiwa amelewa.

Beki huyo wa kulia wa zamani wa Brazil, Cicinho, aliichezea Real Madrid kwa miezi 18 kabla ya kwenda kujiunga na AS Roma ya Italia, Agosti 2007.

Aliichezea Brazil mara 15 kati ya 2005 na 2006 na alifunga bao moja kwenye soka la kimataifa. Staa huyo alibainisha vitu alivyokuwa akifanya nje ya uwanja kwa kipindi chake alichokuwa kwenye kikosi cha Real Madrid, ambako alitumika kwenye mechi 32 pekee.

Alipozungumza na Ressaca, mtandao wa Kibrazili wa EPTV miaka miwili iliyopita, Cicinho amesema alikuwa kwenye vita kali ya kupambana na unywaji wa pombe alipokuwa Madrid.

STA 01

Sasa akiwa na umri wa miaka 45, Cicinho anasema: “Kama watauliza kwamba nilikuwa naenda mazoezini Real Madrid nikiwa nimelewa, ni kweli nilifanya hivyo. Nilikuwa nakunywa kahawa ili kuondoa harufu ya pombe na nilikuwa najipulizia pafyumu. Katika kazi tangu kama mwanasoka wa kulipwa, ilikuwa rahisi, sikuhitaji kuwa na pesa ili kupata pombe.”

Kuhusu ishu ya kuangukia kwenye ulevi, Cicinho amesema: “Nilipokuwa na umri wa miaka 13, nilianza kujaribu pombe kwa mara ya kwanza na tangu kipindi hicho sikuacha. Nilikuwa naishi kijiji na kila ilipofika wikiendi tulikwenda kukutana na marafiki kwenye kumbi za starehe.”

“Nilikuwa nawatuma watu wakubwa kwenda kuninunulia pombe na nilikuwa nakunywa kwa siri ili kuwaficha wazazi wangu na polisi. Nina mtoto wa miaka 15 na kila siku nimekuwa nikimwomba anisamehe.”

STA 02

Ukiweka kando pombe, Cicinho amesema: “Pia nilikuwa navuta sana sigara. Nilivuta sigara kwa miaka 11 kutoka 1999 hadi 2010. Nilikuwa navuta sigara kila wakati ninapokunywa pombe, sasa hebu fikiri nilikuwa navuta kiasi gani kwa sababu nilikuwa nakunywa bia siku nzima.”

Baada ya kujinasua kutoka kwenye janga hilo la ulevi, Cicinho, ambaye alistaafu soka 2018 kwa sasa amejiweka mstari wa mbele katika kuwasaidia wengine kujiepusha na majanga kama hayo.