Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ancelotti: Nina imani kubwa na Alonso pale Real Madrid

CARLO Pict

Muktasari:

  • Ancelotti aliachana na Real Madrid mwishoni mwa msimu uliopita na kutimkia Brazil, ambako amekabidhiwa jukumu la kuionoa timu ya taifa ya nchi hiyo, ambayo bado inasaka nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia 2026, zitakazofanyika nchini Mexico, Canada na Marekani.

Kwa mara ya kwanza kocha mkuu wa timu ya taifa ya Brazil, Carlo Ancelotti, amempongeza kocha wa Real Madrid, Xabi Alonso, huku akimtabiria mambo mazuri katika utendaji wake wa kazi huko Santiago Bernabeu.

Ancelotti aliachana na Real Madrid mwishoni mwa msimu uliopita na kutimkia Brazil, ambako amekabidhiwa jukumu la kuionoa timu ya taifa ya nchi hiyo, ambayo bado inasaka nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Dunia 2026, zitakazofanyika nchini Mexico, Canada na Marekani.

Alonso alichukua nafasi ya Ancelotti kama kocha wa Real Madrid miezi michache iliyopita na tayari ameshaiongoza timu hiyo katika mechi 11, akishinda 10, sare moja na kupoteza moja, huku ikishika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa La Liga.

Akizungumza kuhusu Alonso, Ancelotti amemwambia mwaandishi wa habari wa Hispania, Tomás Roncero, kwamba ana imani Mhispaniola huyo atafanya kazi nzuri na kuendeleza mafanikio ndani ya klabu hiyo yenye maskani yake Santiago Bernabeu.

CAR 01

“Xabi atafanikiwa sana. Nilimwona akiwa Bayern kama mchezaji, ana sifa ya kujituma bila kuchoka na mwenye maono makubwa. Ninaamini hata katika kipindi hiki akiwa kama kocha atafanya vizuri… na kweli kwa sasa anafanya vizuri sana,” amesema Ancelotti kupitia AS.

“Bila shaka, ndiyo. Naona Real Madrid ni imara, hasa eneo la ulinzi, na safu ya ushambuliaji imekuwa na ufanisi zaidi. Mbappé anafanya vizuri, na Bellingham amerudi katika ubora wake. Nadhani Xabi anaweza kufanikisha malengo ta Real Madrid bila shida yoyote.”

Ikumbukwe kuwa, Ancelotti amewahi kuwa kocha wa Alonso wakati wote walipokuwa Bayern Munich ya Ujerumani.

Carlo Ancelotti alianza kuiongoza Real Madrid kwa mara ya pili Juni 2021, akirejea klabuni hapo baada ya kipindi chake cha kwanza cha mafanikio kilichomalizika mwaka 2015. Katika kipindi cha pili, Ancelotti aliiongoza timu hiyo kwa mafanikio makubwa, akirekebisha mchanganyiko wa wachezaji vijana na wazoefu ili kuhakikisha timu ina nguvu ya ushindani katika mashindano yote.

ANC 02

Msimu wa kwanza wa Ancelotti 2021-2022, alifanikiwa kutwaa ubingwa wa LaLiga, na Real Madrid pia ikiibuka kidedea kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. 

Kocha huyo kutoka nchini Italia, aliijenga timu yenye mchanganyiko mzuri wa ushindani na kujenga safu kali ya ushambuliaji iliyokuwa na nguvu, huku akitoa nafasi kwa wachezaji kama Vinícius Jr, Eduardo Camavinga, na Federico Valverde kuonyesha uwezo wao.

Mbali na mafanikio hayo, Ancelotti alihakikisha kwamba timu ilikuwa imara kijiografia na kiakili, ikithibitisha kuwa inaweza kushindana katika mashindano yote, ikiwemo Copa del Rey na Super Cup ya Hispania. 

Carlo Ancelotti aliondoka Real Madrid, Juni 2023, akiacha urithi wa timu iliyo na nidhamu, mchanganyiko wa wachezaji wachanga na wazoefu, na historia ya ushindi wa kimataifa. Urithi wake ulijumuisha uongozi thabiti, mafanikio makubwa ya mashindano, na uthubutu wa kubadilisha timu kuwa mashujaa wa Ulaya na Hispania.