Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbeumo achaguliwa timu Man United, Spurs

MBEUMO Pict

Muktasari:

  • Man United ina matumaini makubwa ya kumnasa mshambuliaji huyo wa Brentford kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi huko Ulaya ikijiandaa kutoa Pauni 60 milioni kumsajili baada ya kukamilisha dili la Matheus Cunha kutoka Wolves.

LONDON, ENGLAND: STAA Bryan Mbeumo ametakiwa achague kwenda Tottenham Hotspur badala ya Manchester United baada ya vita ya miamba hiyo kuwania saini yake kuzidi kupamba moto.

Man United ina matumaini makubwa ya kumnasa mshambuliaji huyo wa Brentford kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi huko Ulaya ikijiandaa kutoa Pauni 60 milioni kumsajili baada ya kukamilisha dili la Matheus Cunha kutoka Wolves.

Hata hivyo, Spurs nayo imeingia kutaka kumsajili Mbeumo ili akakipige London.

 Kocha wa Brentford, Thomas Frank, anatarajia kwenda kurithi mikoba ya Ange Postecoglou huko Spurs wiki ijayo.

Na kinachoelezwa ni kwamba kocha Frank anamtaka Mbeumo wakaungane pamoja huko Spurs, licha ya Mcamerooni huyo kuwa kwenye mazungumzo ya kina ya kutua Old Trafford.

Kutokana na hilo, Mbeumo sasa ana shughuli pevu ya kufanya uamuzi, huku Man United ikimwaandalia dili tamu kabisa, wakati Spurs wao watampa fursa ya kucheza kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na atakwenda kuungana na kocha wake Frank. Na kipa wa zamani wa Man United, Ben Foster ameshangaza wengi baada ya kumshauri Mbeumo akajiunge na Spurs badala ya kwenda Old Trafford. Foster, ambaye aliichezea Man United kati ya mwaka 2005 na 2010, anaamini Spurs ni mahali mwafaka kwa mchezaji huyo kwenda kupata mafanikio makubwa akiwa chini ya kocha wake wa zamani, Frank.

“Ninachoweza kusema kama unataka kuwa sehemu ya kukufanya kuwa bora na kupambana kwa ajili ya kupata kitu kikubwa kwenye timu, basi aende Spurs kufanya kazi na Thomas Frank,” alisema Foster.

“Kama utafurahia kulipwa mshahara mkubwa huku ukijua utakwenda kuwa na presha kubwa, kila mtu anakuanfalia wewe na watu wote watahukumu kwa makosa yako, basi aende Manchester United.”

Mbeumo amekuwa gumzo kwenye Ligi Kuu England na kusakwa na timu nyingi baada ya kufunga mabao 20 msimu uliopita. Asisti zake saba zilikuwa msaada mkubwa kwa Brentford kumaliza nafasi 10 za juu kwenye msimamo wa Ligi Kuu England. Mbeumo amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake huko Brentford ambao una kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi. Man United imemwaandalia mshahara wa Pauni 150,000 kwa wiki, ambao utaongezeka na kufikia Pauni 200,000 kwa wiki kutokana na bonasi, wakati Spurs yenyewe ofa yao ya mshahara ni Pauni 130,000 kwa wiki.