Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mbele ya Beckham, Bolt... Hispania yaandika historia

BECKHAM Pict

Muktasari:

  • Miongoni mwa waliokuwapo uwanjani ni nahodha wa zamani wa England, David Beckham, aliyefuatana na mkewe Victoria Beckham pamoja na watoto wao Cruz, Romeo na Harper.

DALLAS, MAREKANI: NYOTA mbalimbali wa michezo na burudani walijitokeza kushuhudia ushindi wa Hispania wa mabao 2-0 dhidi ya Ufaransa katika nusu fainali ya Kombe la Dunia 2026, huku timu hiyo ikiendelea kuandika historia kwa rekodi zake za kuvutia zilizoipeleka fainali.

Miongoni mwa waliokuwapo uwanjani ni nahodha wa zamani wa England, David Beckham, aliyefuatana na mkewe Victoria Beckham pamoja na watoto wao Cruz, Romeo na Harper.

Nahodha huyo alikuwa miongoni mwa wageni mashuhuri waliohudhuria mchezo wa nusu fainali kati ya Hispania na Ufaransa jijini Dallas.

Beckham, ambaye aliichezea klabu ya Real Madrid ya Hispania kwa miaka minne kuanzia 2003 hadi 2007, alifika uwanjani akiwa ameambatana na familia yake.

BECK 01

Haikuwa mara ya kwanza kwa nyota huyo wa zamani wa England kuhudhuria mchezo wa Kombe la Dunia, kwani ameonekana mara kadhaa katika mashindano hayo akishuhudia mechi mbalimbali za hatua za mtoano.

UFA 01

Pia, walikuwepo mashujaa wa Hispania waliotwaa Kombe la Dunia mwaka 2010 akiwemo Xavi, Sergio Ramos, Iker Casillas na Carles Puyol, walioonekana wakifurahia ushindi wa kizazi kipya cha taifa lao.

Kutoka ulimwengu wa riadha walionekana mabingwa wa mbio za kasi Usain Bolt na Noah Lyles, huku waigizaji maarufu Timothee Chalamet na Javier Bardem nao wakiwa sehemu ya mashabiki waliohudhuria pambano hilo lililopigwa jijini Dallas.

Usain Bolt ni mwanariadha mkongwe kutoka Jamaica anayetambuliwa kama mtu mwenye kasi zaidi kuwahi kuishi, anashikilia rekodi za dunia za mbio za mita 100 (sekunde 9.58) na mita 200 (sekunde 19.19) na ameshinda medal inane za dhahabu kwenye Michezo ya Olimpiki.

UFA 02

Mbele ya mashuhuda hao, Hispania iliendeleza rekodi yake ya kutofungwa baada ya kuiondoa Ufaransa na kutinga fainali ikiwa katika kiwango kinachowafanya wengi kuitaja kama timu yenye nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa.

Kocha wa Hispania, Luis de la Fuente, amesema kikosi chake kimefikia kiwango bora katika wakati muhimu zaidi wa mashindano.

“Wachezaji wangu wanafikia kiwango bora kabisa kwa wakati sahihi,” amesema baada ya mchezo.

BECK 02

Licha ya kuanza kampeni zake kwa sare tasa dhidi ya Cape Verde, Hispania imebadilika kwa kiasi kikubwa, ikishinda mechi sita mfululizo, kufunga mabao 13 kupitia wafungaji saba tofauti na kuruhusu bao moja pekee. Mbali na mafanikio hayo ya timu, kiungo Fabi¡n Ruiz ameendelea kuandika historia binafsi baada ya kufikisha mechi 49 akiwa na timu ya taifa bila kupoteza hata mmoja, rekodi inayozidi kuonyesha uimara wa kizazi hiki cha Hispania.

Aidha, ushindi huo umeifanya Hispania kufikisha mechi 37 mfululizo bila kupoteza katika mashindano yote tangu ilipopoteza dhidi ya Colombia  Machi 2024, rekodi inayolingana na ile ya Italia kati ya mwaka 2018 na 2021.

Mwenendo huo umeamsha kumbukumbu za safari ya Hispania ya mwaka 2010 ilipotwaa Kombe la Dunia licha ya kuanza vibaya,

Imenadikwa na Noor Shija kwa msaada wa mtandao