Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maxey atinga top 5 mastaa wanaowania MVP 2025/26

Muktasari:

  • Msimu huu ulipoanza kulikuwa na uwezekano kwamba Maxey angekuwa mchezaji wa Philadelphia 76ers anayezungumziwa zaidi kwenye vita ya kuwania tuzo hiyo ambayo uliopita ilinyakuliwa na Shai Gilgeous-Alexander wa Oklahoma City Thunder.

OKLAHOMA, MAREKANI: MLINZI nyota wa Philadelphia 76ers, Tyrese Maxey amecheza kwa kiwango bora msimu mzima na wiki hii ameingia katika kinyang'anyiro cha mastaa watano wanaowania ile nafasi ya mchezaji bora (MVP) wa msimu wa 2025/26 katika Ligi ya Kikapu Marekani.

Msimu huu ulipoanza kulikuwa na uwezekano kwamba Maxey angekuwa mchezaji wa Philadelphia 76ers anayezungumziwa zaidi kwenye vita ya kuwania tuzo hiyo ambayo uliopita ilinyakuliwa na Shai Gilgeous-Alexander wa Oklahoma City Thunder.

Kufikia sasa ikiwa ni katikati ya msimu hakuna mjadala wowote upande wa 76ers zaidi ya Maxey, akiwa ameonyesha kuimarika miongoni mwa walinzi wa NBA, na pia namna Joel Embiid na Paul George wenye wasifu mkubwa  walivyotupwa mbali katika mpangilio wa timu hiyo.

Embiid ni mshindi wa zamani wa MVP, na George aliwahi kumaliza wa tatu kwenye kura za kuwania tuzo hiyo, lakini kwa 76ers hivi sasa ni Maxey. Embiid ndi kwanza anarudi kwenye kiwango chake baada ya kusumbuliwa na majeraha sugu ya mguu, huku George akiendelea kuhangaika kurejesha hadhi yake ya zamani ya All-Star.

hata hivyo, wakati wakongwe hao wakisuasua Maxey alijiimarisha katika timu akifunika mabonde ya kaka zake tangu mchezo wa kwanza wa msimu huu, na ni ngumu kumzuia anapodriboli kwani anaweza kukabiliana na mabeki bora, na utupiaji wake mipira akiwa nje ya eneo la wapinzani umeimarika.

Zaidi ya hapo ni uwezo wake wa kutengeneza nafasi kwa wenzake. Kiasili Maxey, ni mfungaji aliye ndani ya mwili wa 'point guard' mwenye urefu wa futi 6 na inchi 2, lakini ana wastani wa asisti  6.7 kwa kila mchezo kikiwa ni kiwango cha juu zaidi katika taaluma yake jambo linaloonyesha ukuaji na ukomavu wake katika msimu wake wa sita.

Kwa hali isiyo ya uhakika ya wachezaji wenzake wawili wakongwe, hasa swali la afya ya Embiid, hatima ya Sixers iko mikononi mwa Maxey. Na anaonekana kuimudu vizuri nafasi hiyo akiwa namba tatu kwa ufungaji NBA nzima kwa dakika anazocheza kwa mchezo.Pia anashika nafasi ya pili kwa uporaji wa mpira kwa kila mchezo.

Nyota huyo yupo ndani ya 'top 15' kwa asisti na amechaguliwa kuanza mchezo wa All-Star msimu, akiwa kwenye mbio za kuchaguliwa timu ya All-NBA. Kwa sasa amekuwa akionekana mara kwa mara kwenye mbio za wanaowania MVP, lakini wiki hii ametinga top 5 akishika nafasi ya tano.

Katika ushindi dhidi ya Houston Rockets wiki hii, Maxey alifunga pointi 17 kati ya 36 alizotupia katika robo ya nne na muda wa nyongeza. Pia alipora mpira katika dakika za mwisho na kutoa asisti mara 10. Ingawa Embiid pia aling’ara kwa 'triple-double' ya pointi 32, mshindi huyo wa zamani wa MVP alimwachia Maxey majukumu muhimu katika mashambulizi ya dakika za mwisho.

76ers wamerekodi ushindi mara 24 na vipigo 19 juu ya mstari wa timu sita za kufuzu mchujo kutokana na uimara na uwezo wa Maxey, lakini ni wazi kwamba atahitaji msaada ikiwa timu hiyo inataka kuendelea kuwa kwenye ushindani.

TOP 10 WANAOWANIA NBA MVP 2025/26

1. Shai Gilgeous-Alexander (Oklahoma City Thunder)

2. Nikola Jokic (Denver Nuggets)

3. Luka Doncic (Los Angeles Lakers)

4. Victor Wembanyama (San Antonio Spurs)

5. Tyrese Maxey (Philadelphia 76ers)

6. Jaylen Brown (Boston Celtics)

7. Cade Cunningham (Detroit Pistons)

8. Anthony Edwards (Minnesota Timberwolves)

9. Alperen Sengun (Houston Rockets )

10. Jamal Murray (Denver Nuggets)