Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maurizio Sarri apasuliwa moyo

SARRI Pict

Muktasari:

  • Klabu yake anayoinoa kwa sasa Lazio inaamini Sarri, 66, atapona kwa haraka na kurudi kwenye majukumu yake haraka.

ROME, ITALIA: ALIYEKUWA kocha wa Chelsea, Maurizio Sarri amefanyiwa upasuaji wa moyo huko Rome, Italia baada ya kupimwa na kuonekana upumuaji wake hauko kawaida.

Klabu yake anayoinoa kwa sasa Lazio inaamini Sarri, 66, atapona kwa haraka na kurudi kwenye majukumu yake haraka.

Kocha huyo Mtaliano, Sarri anayesifika sana kwa kuvuta sigara alipimwa na kukutwa na shida kwenye moyo, ambapo tatizo alilonalo linasababisha uchovu, kizunguzungu, ugumu wa kupumua na kujiweka kwenye hatari ya kupatwa na kiharusi.

“SS Lazio inathibitisha kocha Maurizio Sarri amefanyiwa upasuaji huko Tor Vergata Polyclinic baada ya kukutwa na tatizo kwenye moyo,” ilibainisha taarifa ya Lazio.

“Upasuaji umefanywa na Professor Andrea Natale, mtaalamu wa kimataifa mwenye uzoefu wa zaidi ya miaka 30 wa tatizo hilo na matokeo yake yalikuwa mazuri.”

Kocha huyo wa zamani wa Napoli amekuwa maarufu pia kwa staili yake ya uchezaji iliyofahamika kama Sarri-ball, aliwahi kuinoa Chelsea kwa msimu mmoja na ni maarufu kwa uvutaji sigara.

Sarri alipoondoka Chelsea alijiunga na Juventus, lakini alifutwa kazi baada ya msimu mmoja. Na baada ya kujiuzulu Lazio, Machi 2025 akisema anakwenda kupumziko, alirudi tena kwenye klabu hiyo ya Rome, Juni na kusaini mkataba wa miaka miwili.

Lazio inashika nafasi ya nane kwenye msimamo wa Serie A kwa sasa licha ya kushindwa kufanya usajili wa maana kwenye dirisha lililopita la majira ya kiangazi kwa kutokuwa na pesa.

Kocha msaidizi, Marco Ianni sasa atasimamia timu hiyo hadi hapo Sarri atakaporejea, huku mechi ijayo ya Lazio itakipiga na Napoli, Jumapili ya Januari 4, 2026.