Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa Man Utd waambiwa tiketi ya Ulaya ni lazima

MASTAA Pict

Muktasari:

  • Mkurugenzi wa soka wa klabu hiyo, Jason Wilcox aliwaambia hilo wachezaji wakati anatangaza uamuzi wa kumfuta kazi Ruben Amorim, Jumatatu iliyopita na kuwaambia msimu huu umeshakuwa na mengi ya kuhuzunisha hadi sasa.

MANCHESTER, ENGLAND: MASTAA wa Manchester United wameambiwa kwamba kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ndio malengo ya timu hiyo kwa msimu huu.

Mkurugenzi wa soka wa klabu hiyo, Jason Wilcox aliwaambia hilo wachezaji wakati anatangaza uamuzi wa kumfuta kazi Ruben Amorim, Jumatatu iliyopita na kuwaambia msimu huu umeshakuwa na mengi ya kuhuzunisha hadi sasa.

Lakini, alijaribu kuwaambia wachezaji hao na kuwahamasisha tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao bado ipo kwenye uwezekano wa kuinyakua kwa kuanzia sasa hadi mwisho wa msimu. Man United kwa sasa inashika nafasi ya sita ikiwa na pointi 32, huku nafasi ya tano kwenye msimamo ikitoa pia nafasi ya kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Chanzo kilibainisha: “Wilcox amezungumza na wachezaji katika siku ya kumwondoa Amorim. Amewaambia msimu umekuwa na huzuni nyingi hadi sasa, lakini amewataka wachezaji kuwa na mshikamano na kujaribu kurudi kwenye viwango bora katika nusu ya pili ya msimu.

“Kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya ndiyo malengo na hilo linawezekana. Huo ndio ulikuwa ujumbe wake.”

Kuondoka kwa Amorim kumetoa fursa kwa kiungo Kobbie Mainoo kuwa na uhakika wa kucheza tena baada ya kuwekwa sana benchini na kocha huyo Mreno. Na chanzo kilibainisha: “Kobbie alikuwa na huzuni nyingi sana chini ya Amorim kwa sababu alidhani ameshaingia kwenye kikosi cha kwanza na kupata nafasi ya kucheza. Ghafla tu Amorim akaanza kumwambia anataka acheze tofauti kabisa, kitu ambacho hakikuwa kikimfanya acheze kwenye ubora wake.”

Mainoo alikuwa tayari kuhama kwa mkopo, lakini sasa mazungumzo yameanzishwa kwa ajili ya kuongezwa mkataba mpya. Mkataba wa sasa wa kiungo huyo unamshuhudia akilipwa Pauni 25,000 kwa wiki.