Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mastaa 21 matatani Ligi Kuu England

MASTAA Pict

Muktasari:

  • Ikiwa zimesalia mechi mbili tu kabla ya kutimikia kwa mechi 19, jumla ya wachezaji 21 wako hatarini ya kukumbana na rungu kwani wote wana kadi za njano nne kila moja.

LONDON, ENGLAND: NYOTA wa Ligi Kuu England watakaofikisha kuonyeshwa kadi za njano tano katika mechi 19 za mwanzo za msimu watafungiwa kucheza mechi moja yaani ile ya 20, inaelezwa.

Ikiwa zimesalia mechi mbili tu kabla ya kutimikia kwa mechi 19, jumla ya wachezaji 21 wako hatarini ya kukumbana na rungu kwani wote wana kadi za njano nne kila moja.

Ikiwa mmoja kati ya wachezaji hao 21 atapata kadi ya njano mwishoni mwa wiki hii, atakosa mechi zitakazochezwa kati ya Desemba 26 hadi 28, wakati ambao unaweza kuwa mzuri kwake kwani itakuwa ni kipindi cha sikukuu ya Krismasi.

Vilevile kwa mujibu wa kanuni, hata hivyo, mchezaji yeyote atakayefikisha kadi za njano 10 kabla ya kumalizika kwa mechi ya 32 atafungiwa kucheza mechi mbili.

Iwapo mchezaji atafikisha kadi za njano 15 wakati wowote katika msimu, atafungiwa kucheza mechi tatu.

Baadhi ya nyota kutoka timu zinazopambana katika nafasi za juu kwenye Ligi Kuu England wapo katika orodha ya mastaa waliopo katika hatari ya kukosa mechi moja ikiwa wataonyeshwa kadi ya njano wikiendi hii.

MASTA 01

Kiungo wa Arsenal, Martin Zubimendi, atalazimika kuwa makini kwani naye ni miongoni mwa mastaa wenye kadi nne hadi sasa.

Wachezaji wawili wa Manchester City, Gianluigi Donnarumma na Bernardo Silva, nao pia wana kadi nne kila mmoja.

Matt Cash na Boubacar Kamara wa Aston Villa nao wana kadi nne sawa na beki wa Manchester United, Patrick Dorgu.

MASTA 02

Beki wa Tottenham, Pedro Porro, alipata kadi yake ya nne ya njano katika kipigo cha mabao 3-0 dhidi ya Nottingham Forest Jumapili, baada ya kufanya faulo.

Antoine Semenyo, ambaye amekuwa akiwaniwa na klabu kama Tottenham, Man City, Man United na Liverpool, naye ana kadi nne sawa na staa mwenzake wa timu hiyo Alex Jimenez.

Wachezaji wa Nottingham Forest, Morato na Neco Williams, nao wako hatarini, pamoja na kiungo wa Newcastle, Bruno Guimaraes, Dominik Szoboszlai wa Liverpool na James Garner wa Everton.

MASTA 03

Granit Xhaka wa Sunderland, Nathan Collins wa Brentford, pamoja na wachezaji wa Leeds, Jayden Bogle na Ethan Ampadu, nao wako hatarini.

Vilevile wachezaji wawili wa Brighton, Ferdi Kadioglu na Mats Wieffer, pamoja na wawili wa Wolves, Andre na Matt Doherty, nao pia wako kwenye hatari kubwa ya kufungiwa.