Prime
Mashine ya mashuti inavyonoa mastaa mazoezini

Muktasari:
- Mambo yamebadilika, kutoka mazoezi ya makipa kupigiwa mashuti na wachezaji wenzao, wachezaji kupigiwa pasi za mashuti ya mbali na wachezaji wenzao ili kuonyesha uhodari wa kutuliza mipira hiyo au kuunganisha kufunga mabao hadi mchakato huo sasa kufanyika kwa kutumia mashine maalumu ya kupiga mashuti.
LONDON, ENGLAND: MAISHA yanakwenda kasi sana. Kwenye viwanja vya mazoezi ya mchezo wa soka teknolojia imeshika hatamu.
Mambo yamebadilika, kutoka mazoezi ya makipa kupigiwa mashuti na wachezaji wenzao, wachezaji kupigiwa pasi za mashuti ya mbali na wachezaji wenzao ili kuonyesha uhodari wa kutuliza mipira hiyo au kuunganisha kufunga mabao hadi mchakato huo sasa kufanyika kwa kutumia mashine maalumu ya kupiga mashuti.
Mashine hiyo ya mashuti mazoezini, inaitwa Ball Launcher Trainer.
Hii ni mashine maalumu inayopiga mashuti kwenye mchezo wa soka kwa ajili ya kusaidia wachezaji mazoezini.

Mashine hiyo ina uwezo wa kupiga mashuti makali yanayoenda kwa mita 55 kwa saa. Kwenye mazoezi, mashine hiyo ya mashuti inaweza kusimamiwa na kocha na imekuwa ikitumia pia rimoti.
Ni kifaa mwafaka na sahihi sana katika kuwasaidia makipa na wachezaji wa ndani mazoezini.
Maeneo mengine, mashine hiyo inaitwa Ball Shooter Mashine na inaitwa kati ya Dola 3,299 hadi Dola 3,638.

Teknolojia safi
Mashine hiyo inaweza kuwa kwenye muundo tofauti na ipo ambayo unaweka mpira mmoja na ipo nyingine ambayo inaweza kuweka mipira mingi na yenyewe itakuwa inapiga mashuti mpira mmoja baada ya mwingine kwa kutofautiana kwa sekunde tatu, tano au nane.
Uzuri wa mashine hiyo ni usahihi wa mashuti yake, kama kipa ndiye anayefanya mazoezi kwa wakati huo, basi atakuwa na kazi ya kukabiliana na mashuti yenye uzito uleule, unayopigwa kwenye eneo hilo ili kuhakikisha anakuwa fiti. Hata kwa wachezaji wa ndani pia, wanapokuwa kwenye mazoezi ya kutuliza mipira au kuunganisha ili kufunga mabao, kama vile mazoezi ya kona au pasi ndefu, wanaweza kutumia mashine hiyo, ambayo inapiga mashuti yake kwa usahihi mkubwa. Mashine hiyo inafaa kwa wachezaji wa rika zote na hasa kwa wachezaji wanaojinoa kuwa fiti, huku mashine ikiwafanya wachezaji kuwa wapesi, kwa sababu kama imesetiwa kupiga mashuti kila baada ya sekunde tatu au tano, basi mchezaji husika anapaswa kufanya haraka anapocheza suti la kwanza, ajiendae kwa jingine kwa uharaka.

Uzuri wa mashine hiyo, hasa ile yenye teknolojia ya kisasa, ambayo ina sehemu ya kuweka mipira hadi sita, itakayokuwa inajipiga yenyewe, inamfanya mchezaji awe na uwezo wa kufanya mazoezi kivyake. Mashine inatumia pia rimoti na kipa au mchezaji wa ndani anaweza kuwa na mashine yake binafsi kwa ajili ya kujinoa kuwa matata zaidi.

Uwezo wa mashine
Kwa kifupi, mashine ya mashuti ni kifaa maridhawa cha mazoezi ya makipa, wachezaji wa ndani na timu kwa jumla.
Ina uwezo wa kupiga mashuti zaidi ya 200 kwa usahihi mkubwa ndani ya saa moja.
Inatumika kwenye mipira ya saizi namba 3, 4 na 5 ya mpira wa miguu na kutembewa hewani hadi 55mph.

Inaweza kupiga mashuti kushoto au kulia. Inaweza kupiga mashuti kwa umbali wa mita 33. Na inatumia betri, ambayo inapochagiwa inaweza kukaa na chati kwa zaid ya saa mbili. Betri yake inatoka, hivyo ni rahisi kuchaji na unaweza kuwa na betri ya ziada ili isikuathiri kwenye ufanyaji wa mazoezi yanayohitaji muda unaozidi saa mbili.
Kwenye mazingira ya viwanja vyenye maji vinavyosababisha mpira kuloa maji, inashauriwa mpira huo ufutwe na taulo kwanza kabla ya kuwekwa kwenye mashine ukiwa mkavu ili kupata matokeo sahihi. Haishauriwi kutumia mashinda huyo ya mashuti kwenye mvua za radi au ngurumo. Uzuri wa mashine hiyo haishiki kutu na hata vifaa vyake vyote vinavyotumia umeme vimetengenezwa kwa ukamilifu mkubwa.