Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashabiki waungua moto

Mashabiki Pict
Mashabiki Pict

Muktasari:

  • Mechi hiyo iliyomalizika kwa Stuttgart kufungwa mabao  2-0 iliingia dosari baada ya baruti zilizowashwa katika uwanja huo a kusababisha moshi mzito.

STUTTGART, UJERUMANI: MCHEZO kati ya Stuttgart  na Atalanta uliopigwa katika Uwanja wa MHP Arena, uligubikwa na matukio ya kuungua moto kwa shabiki na kijana mmoja muokota mipira.

Mechi hiyo iliyomalizika kwa Stuttgart kufungwa mabao  2-0 iliingia dosari baada ya baruti zilizowashwa katika uwanja huo a kusababisha moshi mzito.

Moja ya pande za uwanja ulijaa moshi baada ya fataki la rangi  nyekundu wakati wa mchezo na katika kipindi cha pili, miali ya moto ilirushwa kuelekea uwanjani na kumgonga shingoni kijana mmoja muokota mipira.  Taarifa zinaeleza tukio hilo lilirekodiwa kwenye kamera za ulinzi zilizokuwepo uwanjani hapo.

Inaelezwa baada ya kupigwa na miali hiyo madaktari walifika kumtibu na baada kumtoa uwanjani na hadi sasa hakuna taarifa iliyotolewa juu ya hali yake.

Kwa mujibu gazeti la Ujerumani la Welt, shabiki mwingine katika viti alikumbwa na majeraha ya moto, huku wengine wawili wakihitaji matibabu kutokana na kushindwa kupumua baada ya moshi wa mafataki kutanda.

Mbali ya mafataki mengi ambayo yaliwashwa na mashabiki wa wenyeji - Stuttgart, taarifa zinadai hata mashabiki wa timu pinzani pia waliwasha.

Mashabiki wa Stuttgart   wamekuwa wakijulikana kwa tabia hiyo ya kuwasha mafataki wawapo uwanjani ikiwa ni njia mojawapo ya ushangiliaji.

Kwa sasa timu hiyo ambayo ilifanya vizuri msimu uliopita katika Bundesliga baada ya kumaliza nafasi ya pili katika msimamo wa ligi, mambo yake si mazuri na hadi sasa inashika nafasi ya nane ikiwa na pointi 13 baada ya kucheza mechi tisa, ikishinda tatu, sare nne na kufungwa mbili.