Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashabiki, wachezaji wazichapa baada ya timu kupigwa 6-0

MASHABIKI Pict

Muktasari:

  • Mapigano yalizuka nyuma ya goli katika mechi hiyo ya Ligi ya Northern Premier kati ya klabu ya Avro, yenye makao yake Oldham, na Kidsgrove Athletic, Jumamosi mchana Oktoba 18, 2025.

Mechi ya soka ya Northern Premier League Division One West nchini England, imesitishwa baada ya kutokea ugomvi kati ya mashabiki na wachezaji dakika sita kabla ya kumalizika.

Mapigano yalizuka nyuma ya goli katika mechi hiyo ya Ligi ya Northern Premier kati ya klabu ya Avro, yenye makao yake Oldham, na Kidsgrove Athletic, Jumamosi mchana Oktoba 18, 2025.

Mechi hiyo ilisitishwa katika dakika ya 84 huku Avro ikiwa inaongoza kwa mabao 6–0 dhidi ya Kidsgrove iliyokuwa na wachezaji tisa. Katika video iliyosambaa, mchezaji aliyekuwa karibu na goli alionekana kumpiga shabiki. 

Avro imesema kuwa imekasirishwa sana na tukio hilo. Polisi wa Greater Manchester (GMP) wamesema wanachunguza tukio hilo lakini hakuna mtu aliyekamatwa hadi sasa.

Vurugu zilianza baada ya mabishano katika majukwaa, na video zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii zilionyesha wachezaji wa Kidsgrove wakiacha mchezo na kujiingiza katika ugomvi huo.

MASHA 01

Mchezaji mmoja alionekana akiruka vizuizi vya matangazo ili kuingia kwenye majukwaa.

Msemaji wa GMP amesema maafisa wanaendelea kuchunguza mazingira ya tukio hilo. Tukio hilo pia limeripotiwa kwa Shirikisho la Soka (FA).

Katika taarifa yao, Avro wamesema: “Kama klabu, tumekasirishwa sana na tabia ya baadhi ya mashabiki, wachezaji na maofisa wa Kidsgrove Athletic.”

Wameongeza kuwa: “Tukio hilo lilitokea baada ya mmoja wa viongozi wa benchi la Kidsgrove kufukuzwa, ambaye hakuwa uwanjani wakati huo.”

Kwa upande wao, Kidsgrove Athletic wamesema:  “Kama klabu, hatuungi mkono aina yoyote ya tabia isiyofaa. Tumejikita katika kuendeleza heshima na uungwana ndani na nje ya uwanja.”

Wakaongeza kuwa hakuna taarifa zaidi itakayotolewa hadi uchunguzi utakapokamilika.