Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mambo 10 yaliyotokea kipute cha Anfield

ANFIELD Pict

Muktasari:

  • Mechi hiyo iliyomalizika kwa Man United kuichapa Liverpool 2-1, timu zote zilishambuliana kwa zamu na kuonyeshana ubabe kwelikweli uwanjani Anfield.

LIVERPOOL, ENGLAND: MANCHESTER United imesogea kwenye msimamo wa Ligi Kuu England na kuwa nyuma kwa pointi mbili tu kufika kwenye nafasi ya kukamatia tiketi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya ushindi wake muhimu uwanjani Anfield ikiwa ni mara ya kwanza baada ya miaka 10.

Mechi hiyo iliyomalizika kwa Man United kuichapa Liverpool 2-1, timu zote zilishambuliana kwa zamu na kuonyeshana ubabe kwelikweli uwanjani Anfield.

Mfungaji wa bao la ushindi, Harry Maguare alisema: “Hii ni kila kitu. Walikuwa bora dhidi yetu kwa miaka kadhaa, haikuwa nzuri kwa upande wetu. Tulikuwa hatuwapi mashabiki wetu siku nzuri kama hii leo. Hivyo ni kitu tulichokiandaa kwa muda mrefu, kuchukua hizi pointi tatu.”

ANF 05

Nahodha wa zamani wa Man United, Roy Keane alipagawa kwa ushindi huo na kuwataka wachezaji kuchukua hilo kama chachu ya kuendelea kutamba chini ya Ruben Amorim.

Baada ya mechi hiyo kuna vitu hivi hapa 10 vimetokea kutokana na kipute hicho cha Anfield.

ANF 01

1. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Amorim kushinda mfululizo kwenye Ligi Kuu England. Hii ilikuwa mechi yake ya 35 kwenye Ligi Kuu England tangu alipoanza kuinoa timu hiyo.


2. Huu ulikuwa ushindi wa kwanza kwa Man United ugenini dhidi ya Liverpool tangu 2016. Louis van Gaal ndiye alikuwa kocha wakati Man United iliposhinda Anfield kipindi hicho, Jose Mourinho, Ole Gunnar Solskjaer, Ralf Rangnick na Erik ten Hag wote walishindwa Anfield.


3. Liverpool mechi tatu za mwisho kwenye Ligi Kuu England imepata matokeo yanayofanana: inatangulia kufungwa, inasawazisha kisha inaruhusu tena bao na kupoteza 2-1.


ANF 02

4. Jurgen Klopp hajawahi kupoteza mechi nne mfululizo alipokuwa Liverpool. Mara ya mwisho Liverpool kupoteza kwenye mechi nne mfululizo ilikuwa chini ya Brendan Rodgers, 2014.


5. Bryan Mbeumo alifunga bao ambao ni la pili kupatikana mapema kwenye mechi za Liverpool na Man United kwenye Ligi Kuu England. Bao jingine la haraka lilifungwa na Nicky Butt wa Man United pia, Oktoba 1995.


ANF 03

6. Cody Gakpo aligongesha nguzo mara tatu. Ni mara moja tu kwenye rekodi za Ligi Kuu England mchezaji kugongesha nguzo mara nyingi (Darwin Nunez, Liverpool vs Chelsea, Januari 2024).


7. Licha ya kiwango kibovu cha Liverpool kwa sasa, Opta iliipa Liverpool alama kubwa za uwezekano wa kushinda mechi hiyo, asilimia 73.3, wakati kupoteza ilikuwa asilimia 11.2.


ANF 04

8. Bruno Fernandes aliasisti bao la Ligi Kuu England uwanjani Anfield kabla ya Florian Wirtz tangu atue Liverpool.


9. Mchezaji bora wa mechi, Harry Maguire aliibuka mshindi kwenye mipira mitano ya juu na aliokoa hatari nane kabla ya kufunga bao la ushindi. Alikuwa juu kuliko wote Man United.


10. Hiyo ilikuwa mechi ya 100 kwa timu hizo kukutana Anfield. Huo ulikuwa ushindi wa 27 kwa Man United. Liverpool imeshinda 46 na sare 37.