Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mashabiki Liverpool washindwa kuvumilia

MASHABIKI Pict

Muktasari:

  • Liverpool walikuwa ni wageni katika mechi ya robo fainali ya Kombe la FA dhidi ya kikosi cha Pep Guardiola na ikapokea kipigo kizito cha mabao 4-0.

LIVERPOOL, ENGLAND: MASHABIKI wa Liverpool wenye hasira walionekana wakiondoka katika Uwanja wa Etihad wakati mechi kati ya klabu yao na Manchester City  ikiwa imechezwa kwa dakika 60 tu.

Liverpool walikuwa ni wageni katika mechi ya robo fainali ya Kombe la FA dhidi ya kikosi cha Pep Guardiola na ikapokea kipigo kizito cha mabao 4-0.

Kosa la kizembe kutoka kwa Virgil van Dijk dhidi ya Nico O’Reilly liliwapa wenyeji nafasi adhimu ya kufungua bao kwa njia ya penalti, iliyopigwa na  Erling Haaland.

Mshambuliaji huyo wa Norway alifunga tena kwa kichwa, kisha Antoine Semenyo akafunga bao la tatu mwanzoni mwa kipindi cha pili kabla ya Haaland kukamilisha hat-trick yake kwa kufunga bao la nne.

Bao hilo lililowafanya wenyeji kuongoza 4-0 na kusababisha mashabiki wengi wa Liverpool kuanza kuondoka uwanjani.

Mashabiki walimiminika kuelekea milangoni huku wapinzani wao wakishangilia kwa kuwazomea na kuwatania.

Hata hivyo, mashabiki waliobaki walipata matumaini kidogo baada ya timu yao kupewa penalti, hata hivyo, yalizimika pale Mohamed Salah alipopiga penalti dhaifu iliyodakwa kirahisi na kipa James Trafford.

Matokeo hayo mabaya yanakuwa pigo kubwa kwa kocha Arne Slot, ambaye tayari alikuwa chini ya presha kutokana na kiwango kibovu cha Liverpool msimu huu.

Timu yake imepoteza mechi tatu zilizopita za Ligi Kuu England, zikiwemo dhidi ya Wolverhampton Wanderers na Tottenham Hotspur. Mashabiki mara kadhaa wamekuwa wakiimba kutaka kocha huyo afukuzwe.

Kiungo wa zamani wa Liverpool Xabi Alonso ameendelea kuhusishwa kuwa anaweza akaajiriwa kuchukua nafasi ya Slot ikiwa maamuzi ya kumuondoa yatafanyika.