Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Manchester United yafikiria kumuuza Bruno Fernandes

Muktasari:

  • Inaelezwa klabu hiyo inaweza kufikiria kumuuza ikiwa itapokea ofa kubwa kutoka PSG na Bayern Munich ambazo zinatamani sana huduma yake.

HATMA ya nahodha wa Manchester United, Bruno Fernandes, 31, bado ni kizungumkuti wakati huu dirisha la usajili la majira ya kiangazi likikaribia.

Inaelezwa klabu hiyo inaweza kufikiria kumuuza ikiwa itapokea ofa kubwa kutoka PSG na Bayern Munich ambazo zinatamani sana huduma yake.

Hata hivyo, baadhi ya taarifa zinadai Man United ina nia ya kumbakisha kiungo huyo muhimu licha ya taarifa zinazodai katika mkataba wake kuna kipengele kinachoelezea kwamba anaweza akaondoka ikiwa timu inayomtaka italipa Pauni 57 milioni.

Fernandes kwa sasa ni mhimili wa kikosi cha Man United na msimu huu ameonekana kuwa bora zaidi chini ya kocha wa muda, Michael Carrick. Mkataba wa nyota huyo wa kimataifa wa Ureno unatarajiwa kumalizika mwakani. Tangu kuanza kwa msimu huu amecheza mechi 30 za michuano yote.


Elliot Anderson

MANCHESTER United na Manchester City zinataka kukamilisha haraka usajili wa kiungo wa kimataifa wa  England, Elliot Anderson, 23, anayekipiga katika Nottingham Forest. Sababu kubwa ya kutaka kufanya  haraka inatajwa kuwa ni hofu ya thamani ya mchezaji huyo inaweza kupanda hadi zaidi ya Pauni 100 milioni  iwapo atafanya vizuri katika Kombe la Dunia akiwa na timu ya taifa ya England. Staa huyu ameonyesha kiwango bora msimu huu.


Khephren Thuram

LIVERPOOL inaweza kukutana na ushindani mkali kutoka Manchester United  na Newcastle United  katika mbio zao za kumsajili kiungo wa Juventus na timu ya taifa ya Ufaransa, Khephren Thuram, 25, katika dirisha lijalo. Thuram anaendelea kuvutia kutokana na uwezo wake wa matumizi makubwa ya  nguvu na ubunifu, jambo linalomfanya kuziaminisha klabu za England kwamba atawasaidia sana. Nyota huyo yupo katika rada ya timu kibao.


Marcos Senesi

BEKI wa kati wa Argentina, Marcos Senesi, 28, anayeichezea Bournemouth, anatamani kujiunga na Barcelona katika dirisha la usajili la majira ya kiangaz. Hata hivyo, huduma yake pia inahitajika na klabu kadhaa za England ikiwemo Liverpool, Chelsea, Aston Villa, Everton, Tottenham Hotspur, Newcastle United na Sunderland. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika ifikapo mwisho wa msimu.


Karim Coulibaly

BEKI kinda wa kimataifa wa Ujerumani, Karim Coulibaly, 18, anajiandaa kuondoka Werder Bremen katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Inaelezwa kuwa Newcastle United ni miongoni mwa klabu tano zinazomuwania beki huyo chipukizi, ambaye ameaonyesha kiwango bora msimu huu kutokana na uwezo wake licha ya umri mdogo. Iwapo ataondoka, Coulibaly anaweza kuwa moja ya wachezaji wadogo wanatakaouzwa kwa pesa nyingi.


Jhon Lucumi

BEKI wa kimataifa wa Colombia, Jhon Lucumi, 27, anaonekana kuwa karibu kuondoka Bologna katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Inaelezwa Sunderland  bado inaonyesha nia ya kumsajili beki huyo, baada ya kushindwa kumpata katika jaribio lao la awali miezi kadhaa  iliyopita. Lucumi ndio beki kiongozi wa safu ya ulinzi ya Bologna, lakini amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya mara kwa mara. Msimu huu amecheza mechi 35.


Bart Verbruggen

KIPA wa kimataifa wa Uholanzi, Bart Verbruggen, 23, anayekipiga Brighton anaweza kuwa chaguo la usajili wa kipa wa Bayern Munich katia dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Mbali na Bayern, klabu kama Tottenham Hotspur na Newcastle United zinazohitaji kusajili kipa mwisho wa msimu, zinamfuatilia kwa karibu. Verbruggen anachukuliwa kama mmoja wa makipa bora Ulaya kwa sasa.


Moises Caicedo

KIUNGO wa kimataifa wa Ecuador, Moises Caicedo, 24, amesisitiza kwamba bado anatamani kuendelea kuitumikia Chelsea kwa muda mrefu zaidi na hana mpango wa kuondoka kwa sasa. Hata hivyo, baadhi ya taarifa zinaeleza Chelsea haitofikiria mara mbili ikiwa itapokea ofa nono ya kumuuza kiungo huyo kwenda timu nyingine kubwa nje ya England. Caicedo ana mkataba kuitumikia Chelsea hadi 2031.