Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Maneno ya Cristiano Ronaldo yaungwa mkono na Novak Djokovic 

DJOKOVIC

Muktasari:

  • Ronaldo aliandika ujumbe kwenye mitandao ya kijamii akieleza siku zote mafanikio sio bahati, akimaanisha kupambana zaidi kunaakisi mafanikio ya kweli, na sio kutegemea bahati, kama watu wengi duniani wanavyoamini.

Nyota wa Tenisi, Novak Djokovic amempongeza nahodha na mshambuliaji wa Al NAssr ya Saudi Arabia, Cristiano Ronaldo kwa kauli yake kuhusu kupambana na kupata mafanikio.

Ronaldo aliandika ujumbe kwenye mitandao ya kijamii akieleza siku zote mafanikio sio bahati, akimaanisha kupambana zaidi kunaakisi mafanikio ya kweli, na sio kutegemea bahati, kama watu wengi duniani wanavyoamini.

Djokovic, amekubaliana na kauli hiyo ya Ronaldo, kwa kusema ni kweli mafanikio hayapatikani kwa bahati, siku chache baada ya kumtaja mshambuliaji huyo kutoka Ureno kuwa mmoja wa watu wanaompa motisha kubwa katika maisha yake ya michezo.

Ronaldo aliweka wavuni bao kali wakati Al-Nassr ikiibuka na ushindi wa 5-1 dhidi ya Al-Fateh kwenye Ligi Kuu ya Saudi Arabia (Saudi Pro League), juzi Jumamosi, Oktoba 18, 2025. 

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 40, alifunga kwa shuti kali kutoka nje ya boksi dakika ya 60, muda mfupi baada ya kukosa penalti. Pia alitoa pasi ya bao kwa Joao Felix, ambaye alipiga hat-trick katika mechi hiyo.

Baada ya ushindi huo mnono, Ronaldo aliposti kwenye mitandao ya kijamii ujumbe mzito: "Mafanikio si bahati."

DJOKO 01

Djokovic hakusita kuonesha kuunga mkono kauli hiyo. Kupitia Instagram Story yake, alishiriki chapisho la Ronaldo, akiambatanisha emoji ya mkono wenye nguvu 💪 na mikono miwili iliyoinuliwa 🙌, kuonesha kumuunga mkono.

Siku chache kabla tukio hilo, Djokovic alikuwa ameieleza BBC kuwa Ronaldo ni moja ya vyanzo vyake vya msukumo, hasa anapotazama wachezaji wanaodumu kwa muda mrefu katika viwango vya juu vya michezo.

"Uvumilivu wa muda mrefu ni moja ya sababu zinazonisukuma. Natamani kuona ni kwa muda gani nitaweza kuendelea kucheza," amesema Djokovic.

"Ukitazama michezo mikubwa duniani, utagundua LeBron James, bado anacheza akiwa na miaka 40, Cristiano Ronaldo, Tom Brady alicheza hadi miaka zaidi ya 40, ni jambo la kushangaza. Wanahamasisha sana."

Djokovic mwenye umri wa miaka 38, kwa sasa anashikilia rekodi ya mataji mengi ya Grand Slam kwa wanaume (24), na anawania kuwa na mataji mengi zaidi kuliko mchezaji yeyote (wanaume au wanawake) katika historia ya tenisi.

Kwa upande mwingine, Ronaldo bado anaendelea kung’ara licha ya kuwa kwenye hatua ya mwisho ya kazi yake ya soka, na sasa analenga kufunga jumla ya mabao 1000 katika maisha yake ya soka, lengo la kihistoria ambalo halijawahi kufikiwa na mchezaji yeyote.