Manchester United, Arsenal kusaka rekodi leo

LONDON, ENGLAND. EPL kitawaka tena wikiendi hii ambapo leo Jumamosi kutakuwaa na  michezo sita huku baadhi ya rekodi zikitarajiwa kuwekwa na nyingine kuvunjwa.

Arsenal itakuwa inapambana kuisaka rekodi ya kukaa kwenye kilele cha msimamo wa Ligi Kuu England katika misimu miwili mfululizo katika mzunguko wa 15 na 16.

Arsenal inaikimbizia rekodi yao ya msimu wa 2002/03 na 2003/04 ambapo ilifanikiwa kukaa kwenye kilele cha ligi hiyo katika mizunguko hiyo.

Rekodi zinaonyesha kwamba tangu mwaka 2000, Arsenal ilichukua ubingwa mara moja tu kati ya mara zote ilizokuwa kwenye kilele cha msimamo ndani ya mzunguko wa 15 na 16, hiyo ilikuwa ni mwaka 2003/04 ambao pia ndio ulikuwa ubingwa wake wa mwisho. Arsenal itaisaka rekodi hii itakapokutana na Aston Villa ugenini katika Uwanja wa Villa Park kuanzia saa 2:30 usiku.

Villa ambayo imetoka kuifunga Man City kwa sasa inafundishwa na Unai Emery ambaye aliwahi kuwa kocha wa Arsenal kuanzai mwaka 2018 hadi 2019 kabla hajatimuliwa.

Hadi sasa rekodi zinaonyesha kwamba Arsenal imekutana na Villa mara 56, ikashinda mara 31  huku Villa ikishinda mara 11 na mechi 14 zilimalizika kwa sare.

Mbali ya Arsenal inayokimbizia rekodi hiyo, Man United nayo itakuwa inapambana kutoa gundu kwa kukaa  kwenye nafasi tano za juu katika msimamo kwa mara yakwanza tangu kuanza kwa msimu huu.

Vilevile itakuwa inahitaji kushinda ili kufikisha alama 30 sawa na majirani zao Manchester City ambao msimu huu wameonekana kuwa na panda shuka nyingi baada ya kuchukua mataji matatu msimu uliopita.

Man United inayoshikilia nafasi ya sita itakutana na Bournemouth ambayo kama ikishinda pia inaweza kwenda kuishusha Chelsea kwasababu itafikisha alama 19 sawa na matajiri hao wa London ambao hadi sasa wanashika nafasi ya 10 kwenye msimamo.

Man United na Bournemouth kwaujumla zimekutana mara 12 kwenye historia ya EPL na Man United imeshinda mara tisa huku Bournemouth ikishinda mara mbili na mchezo mmoja kumalizika kwa sare.

Mara yamwisho Bournemouth kushinda dhidi ya Mashetani Wekundu ilikuwa mwaka 2019.

Mbali ya Arsenal na Man United kutakuwa na mchezo wa mapema kati ya Crystal Palace na Liunaotarajiwa kupigwa saa 9:30, mechii pia inatolewa macho kwa sababu Liverpool ikishinda itaishusha Arsenal  kwenye msimamo wa EPL ikiwa itapoteza dhidi ya Villa.

Msimamo unaonyesha Arsenal ina pointi 36 wakati Liverpool ina pointi 34, ikiwa Arsenal itapigwa na Liverpool ikishinda itafikisha alama 37.  Vilevile Wolves itaumana na Nottingham Forest saa 12:00 jioni huku Brighton ambayo itakuwa nyumbani itaumana na Burnley muda kama huo.