Manchester City yamwania kipa namba moja wa Napoli

Muktasari:

Manchester City tayari imemsajili kipa wa Benfica, Ederson Moraes kwa dau la Pauni 34 milioni wakati mlinda wake mwingine Willy Caballero amejiunga na Chelsea kwa uhamisho huru na Joes Hart anakaribia kusajiliwa na klabu ya West Ham.

London, England. Manchester City imekamia kumsajili kipa wa zamani wa Liverpool, Pepe Raina kutokana na aliyepo sasa Claudio Bravo kukaribia kuondoa kwenye dimba la Etihad.

Manchester City tayari imemsajili kipa wa Benfica, Ederson Moraes kwa dau la Pauni 34 milioni wakati mlinda wake mwingine Willy Caballero amejiunga na Chelsea kwa uhamisho huru na Joes Hart anakaribia kusajiliwa na klabu ya West Ham.

Gazeti a Telegram liliripoti kuwa, Manchester City inajiandaa kuongeza dau la Pauni 4.4 milioni baada ya lile la awalia la Pauni 2.6 kukataliwa ili kumpata kipa huyo wa Napoli.

Iwapo mazungumzo yatafikiwa wiki hii, itatumia nguvu zake kumsajili Raina (33) ambaye ni kipa namba moja wa Napoli.