Manchester City kumalizana na Pep

Muktasari:
- Kocha huyu wa zamani wa Barcelona mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu ujao na Man City ipo tayari kumpa ofa anayohitaji ingawa akiamua kuondoka pia hawatomzuia.
MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER City inataka kumsainisha mkataba mpya kocha wao, Pep Guardiola utakaomwezesha kusalia katika timu huyo kwa miaka 10 au zaidi tangu alipotua mwaka 2016 akitokea Bayern Munich.
Kocha huyu wa zamani wa Barcelona mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu ujao na Man City ipo tayari kumpa ofa anayohitaji ingawa akiamua kuondoka pia hawatomzuia.
Taarida kutoka Daily Mail zinaelewa mazungumzo yanaenda vizuri na una uwezekano kocha huyo raia wa Hispania akaendelea kuwepo kwa muda mrefu zaidi.
Mbali ya mabosi hata wachezaji pia wanahitaji kocha huyo abaki ingawa uamuzi sasa ni wake.
Iwapo Guardiola ataamua kuongeza mkataba, ataendelea kuifundisha timu hiyo kwa msimu ujao na watakuwa katika uchunguzi unaoendelea juu ya mashtaka 115 ya ukiukaji wa sheria za matumizi ya pesa.
Jumapili, vijana wa Guardiola waliwashinda West Ham na kutwaa taji la sita la ligi ya juu katika Gauardiola ameiwezesha timu hii kushinda taji la nne mfululizo la Ligi Kuu England msimu huu baada ya kupata ushindi katika mchezo wa mwisho dhidi ya West Ham.
Ilikuwa ashinde na FA lakini mambo yakaenda kombe na kupoteza mbele ya wapinzani wao Man United kwa mabao 2-1.
Katika mechi ya mwisho ya msimu dhidi ya West Ham, alipoulizwa juu ya kubaki ama kuondoka, alisema
“Ukweli ni kwamba niko karibu kuondoka kuliko kubaki, ila nimezungumza na klabu na nimewaambia nataka kubaki hadi mkataba wangu utakapomalizika kisha tutazungumza.”