Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

De Bruyne aandaliwa mechi yake Etihad

ETIHAD Pict

Muktasari:

  • Mechi hiyo itakuwa ya mwisho kwa Man City kucheza kwenye uwanja wao wa nyumbani, Etihad na itapigwa Jumanne, Mei 20.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER City imefichua mechi yao dhidi ya Bournemouth itakayopigwa baadaye mwezi huu itakuwa maalumu kwa ajili ya kumuaga kiungo wao, Kevin De Bruyne.

Mechi hiyo itakuwa ya mwisho kwa Man City kucheza kwenye uwanja wao wa nyumbani, Etihad na itapigwa Jumanne, Mei 20.

Mwanzoni mechi hiyo ilipangwa kufanyika wikiendi, lakini Man City inakabiliwa na fainali ya Kombe la FA dhidi ya Crystal Palace, hivyo ratiba ya mechi hiyo ilibadilishwa. Mechi hiyo itakuwa ya mwisho nyumbani na imepangwa kuwa maalumu kwa ajili ya De Bruyne, ambaye ataachana na miamba hiyo mwishoni mwa msimu.

Man City imemfungulia milango ya kutokea Mbelgiji huyo mwishoni mwa msimu wakati mkataba wake utakapofika tamati, muongo mmoja tangu alipoanza kuitumikia. De Bruyne, 33, ataondoka Man City akiwa ameshinda mataji sita ya Ligi Kuu England, huku akichaguliwa pia Mchezaji Bora wa Mwaka wa PFA mara mbili tofauti. De Bruyne ataagana na mashabiki baada ya mechi.

Taarifa ya klabu ya Man City ilisomeka: "Hii ina maana mechi ya Bournemouth itakuwa yenye hisia kubwa kwa mashabiki, makocha na wachezaji kwa sababu inatoa nafasi ya kuadhana na King Kev kwa sababu ya kile alichofanya tangu alipojiunga hapa 2015.

"Kutakuwa na utambulisho baada ya mechi na Kevin atakuwa na nafasi ya kuzungumza na mashabiki kwa mara ya mwisho kwa wale watakaokuwa uwanjani Etihad."

De Bruyne amekuwa na msimu wenye majeruhi mengi na hivyo kushindwa kuisaidia timu ya Man City kutetea ubingwa wa Ligi Kuu England, ambao sasa umebebwa na Liverpool. Mkataba wake utafika tamati mwishoni mwa Juni mwaka huu.