Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United yaweka mambo hadharani kuhusu Ten Hag

Muktasari:

  • Ten Hag alifukuzwa na Man United Oktoba mwaka jana baada ya kushinda mechi tatu tu kati ya tisa za mwanzo za Ligi Kuu England.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER UNITED imefichua ni kiasi gani ilichotumia kama fidia ya kumfukuza Erik ten Hag na Dan Ashworth huku deni lao likifikia Pauni 1 bilioni.

Ten Hag alifukuzwa na Man United Oktoba mwaka jana baada ya kushinda mechi tatu tu kati ya tisa za mwanzo za Ligi Kuu England.

Baada ya kuondoka kwake Man United pia iliwafuta kazi makocha wengine waliokuwa wanafanya naye kazi ili kumpisha Ruben Amorim na benchi lake.

Mbali ya Ten Hag na benchi lake, Desemba pia ilitangazwa mkurugenzi wa michezo Ashworth angeondoka baada ya miezi mitano tu ya kazi hiyo.

Katika ripoti ya kifedha ya robo ya pili ya mwaka wa 2025 yaliyochapishwa jana, ilionekana Man United ilitumia kati ya Pauni 10.4 hadi Pauni 14.5 milioni kumfukuza Ten Hag na wafanyakazi wake na ikatumia Pauni 4.1 milioni kumuondoa kwa Ashworth.

Ripoti ya kifedha pia ilionyesha mapato ya klabu yalishuka kwa asilimia 12 kwa robo hiyo na ilisababishwa na upungufu wa asilimia 42.1 katika mapato ya matangazo ambayo yameshuka hadi Pauni 61.6 milioni kutokana na kutokucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Hata hivyo, Man United ripoti inaeleza kulikuwa na ongezeko la mapato ya kibiashara  kwa asilimia 18.5 yaliyochangiwa na udhamini mpya wa jezi kutoka Qualcomm’s Snapdragon brand.

Hesabu pia zikaonyesha mashetani hawa wekundu  walikuwa na faida ya uendeshaji ya Pauni 3.1 milioni, na faida kabla ya riba, kodi, Pauni 70.5 milioni, ikishuka kwa asilimia 22.9 kutoka Pauni 91.4 milioni mwaka wa 2024.

Kwa upande wa biashara ya wachezaji, hii ilileta hasara ya Pauni 27.7 milioni.

Pesa za mfuko wa aiba wa timu zimeongezekana kufikia Pauni 80 milioni kutokana na uwezekezaji wa Ineos na isingekuwa yeye Man  United ingekuwa na akiba ya Pauni 15 milioni pekee.

Deni la timu kabla ya riba jumla linasimama kwenye Pauni 731 milioni,  huku takriban Pauni 300 milioni ikiwa ni pesa za uhamisho wa wachezaji.

Katika taarifa, Mkurugenzi Mtendaji Omar Berrada alizungumzia changamoto zinazoikabili timu hiyo na kazi inavyoendelea katika kutengeneza uwanja wa Old Trafford na kuboresha kituo cha mazoezi cha Carrington.