Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Man United yavunja rekodi chafu tu

Muktasari:


  • Man United ilikubali kipigo cha mabao 3-0 uwanjani Old Trafford na hivyo kushuka hadi nafasi ya 13 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England baada ya mabao ya Dean Huijsen, Justin Kluivert na Antoine Semenyo.

MANCHESTER, ENGLAND: MANCHESTER United imeendelea kukusanya rekodi za hovyo kwenye Ligi Kuu England baada ya kukubali kipigo kutoka kwa Bournemouth juzi Jumapili.

Man United ilikubali kipigo cha mabao 3-0 uwanjani Old Trafford na hivyo kushuka hadi nafasi ya 13 kwenye msimamo wa Ligi Kuu England baada ya mabao ya Dean Huijsen, Justin Kluivert na Antoine Semenyo.

Hicho kilikuwa kipigo kizito zaidi kwa kocha mpya Ruben Amorim, ambaye alichukua mikoba ya timu hiyo kutoka kwa Mdachi, Erik ten Hag baada ya timu kuanza msimu vibaya. Na sasa rekodi mbaya zimeendelea kutokea kwenye kikosi hicho cha Old Trafford.

Man United sasa imejikuta ikiwa kwenye 10 la chini katika msimamo wa Ligi Kuu England wakati wa Krismasi kwa mara ya kwanza katika historia ya ligi hiyo.

Na ukiondoa mabao ya penalti, Man United sasa imeruhusu mabao 17 kutokana na mipira ya kutenga ndani ya mwaka huu kwenye Ligi Kuu England.

Hiyo ni idadi kubwa ya mabao kufungwa ndani ya mwaka mmoja kwenye mikikimikiki ya Ligi Kuu England. Kocha Amorim alibainisha udhaifu wa timu yake katika kujilinda na mipira ya kutenga kwenye mahojiano yake aliyofanya na waandishi kabla ya mechi hiyo.

Amorim alisema: “Ni ngumu sana. Katika hali hii, ni ngumu kupata ushindi kwenye mechi mbili au tatu. Bado tunapambana. Lakini, mechi hii ilikuwa ngumu sana kwetu. Katika hali ileile, tumepata shida tena kwenye mipira ya kutenga. Nadhani tumekuwa na woga kidogo kwenye hilo. Tulijaribu kufunga mabao, lakini mwishowe mambo yanapokuwa magumu yanaweza kubaki kwenye ugumu huo huo. Tunahitaji kusonga mbele.”